Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi. 
 Gari la shirika la umeme Tanzania (Tanesco) imepinduka usiku huu baada ya kugongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Toyota Corola katika eneo la Kwa Sadala barabara ya Moshi/Arusha. 
 Kwa mujubu wa shuhuda wa ajali hiyo, gari la Tanesco lilikuwa limepakia wafanyakazi wa shirika hilo wapatao 18 wakitokea eneo la KIA kuelekea mjini Moshi. 
 Amesema dereva wa gari dogo alikuwa akijaribu kuzipita gari kadhaa zilizokuwa zikielekea Arusha ndipo akakutana na Loli hilo kabla ya kurudi  upande wake.
Ndipo gari magari hayo yakagongana na kisha gari la Tanesco kupinduka. Shuhuda  amesema majerhi wa ajali hiyo walikimbizwa hosptali ya KCMC huku dereva wa gari hilo dogo akiingia mitini na kutokomea kusiko julikana.
Toyota Corola lililosababisha ajali hii
Askari wa usalama barabarani na gari la tanesco lililopinduka
wadau eneo la  tukio

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. ni nyumbani moshi nimesikitika sana

    ReplyDelete
  2. Tanzania madereva wengi wavuta bangi, walevi.......maskini wengi wao wameathirila kisaikolojia hawathamini maisha yao tena

    ReplyDelete
  3. Sina takwimu Sahihi lakini karibu 90% ya ajali zinazotokea highways zinahushisha kuovertake. acheni kuovertake jamani, hasa unapoona huna uhakika na usalama.

    ReplyDelete
  4. Tuwape pole majeruhi na kuwaomba Mamlaka husika zilizokabidhiwa kulinda usalama wa raia na mali zao siyo kufanyakazi mchana tu na kusahau usiku.Nina uhakika kuna mgawanyo wa kazi na ziko shift za usiku na mchana. Binadamu wanajotahidi kuwa wastaarabu mchana lakini hubadilika jua linapokuchwa. Tafadhali Mamlaka husika hakuna haja ya kutukanana wala kuharibiana kazi.Tufanye kazi tutekeleze wajibu wetu kwa jamii. Hii ni amana kwako kwangu na kila mtu.Magari yanaongezeka na barabara zinakuwa nzuri kwahiyo watumiaji lazima wawe na mtiririko sahihi wa kufuatilia. Mimi binafsi nilimpoteza rafiki yangu na mdarasa mwenzangu hapohapo kwa Sadala.Mungu bariki Tanzania na watu wakemAmeen. SAM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...