Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi.
Gari la shirika la umeme Tanzania (Tanesco) imepinduka usiku huu baada ya
kugongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Toyota Corola katika eneo
la Kwa Sadala barabara ya Moshi/Arusha.
Kwa mujubu wa shuhuda wa ajali hiyo, gari la
Tanesco lilikuwa limepakia wafanyakazi wa shirika hilo wapatao 18 wakitokea eneo la KIA kuelekea mjini Moshi.
Amesema dereva wa gari dogo alikuwa akijaribu kuzipita gari kadhaa
zilizokuwa zikielekea Arusha ndipo akakutana na Loli hilo kabla ya kurudi upande wake.
Ndipo gari magari hayo
yakagongana na kisha gari la Tanesco kupinduka. Shuhuda amesema majerhi wa ajali hiyo walikimbizwa hosptali ya KCMC
huku dereva wa gari hilo dogo akiingia mitini na kutokomea kusiko
julikana.
Toyota Corola lililosababisha ajali hii
Askari wa usalama barabarani na gari la tanesco lililopinduka
wadau eneo la tukio
ni nyumbani moshi nimesikitika sana
ReplyDeleteTanzania madereva wengi wavuta bangi, walevi.......maskini wengi wao wameathirila kisaikolojia hawathamini maisha yao tena
ReplyDeleteSina takwimu Sahihi lakini karibu 90% ya ajali zinazotokea highways zinahushisha kuovertake. acheni kuovertake jamani, hasa unapoona huna uhakika na usalama.
ReplyDeleteTuwape pole majeruhi na kuwaomba Mamlaka husika zilizokabidhiwa kulinda usalama wa raia na mali zao siyo kufanyakazi mchana tu na kusahau usiku.Nina uhakika kuna mgawanyo wa kazi na ziko shift za usiku na mchana. Binadamu wanajotahidi kuwa wastaarabu mchana lakini hubadilika jua linapokuchwa. Tafadhali Mamlaka husika hakuna haja ya kutukanana wala kuharibiana kazi.Tufanye kazi tutekeleze wajibu wetu kwa jamii. Hii ni amana kwako kwangu na kila mtu.Magari yanaongezeka na barabara zinakuwa nzuri kwahiyo watumiaji lazima wawe na mtiririko sahihi wa kufuatilia. Mimi binafsi nilimpoteza rafiki yangu na mdarasa mwenzangu hapohapo kwa Sadala.Mungu bariki Tanzania na watu wakemAmeen. SAM
ReplyDelete