Balozi Mulamula akiwasili kwenye park ya Wheaton huku akilakiwa na Afisa Ubalozi Suleiman Saleh.

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Mustafa Nyang'anyi wakiwemo viongozi wa TAMCO na wajumbe wa Jumuiya ya Watanzania DMV.
Mhe.Balozi Liberata Mulamula naye alisisitiza umoja wa Watanzania na kuimwagia sifa Jumuiya ya Waislamu DMV (TAMCO) kwa mshikamano walionao na jitihada zao za kuwaunganisha Watanzania wa DMV bila kujali itikadi za dini zao na kusema kwamba kuanzia jana yeye amejiunga rasmi na atakuwa mwanachama wa kudumu wa TAMCO pia aliwakumbusha enzi ya kidongo chekundu na Zanzibar sikukuu ya Eid ilivyokuwa ikisherehekewa pia alikabidhi Eid yake kwa Afisa Ubalozi Abbas Missana kwa ajili ya  watoto waliokuwepo kwenye sherehe hiyo.
Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Mustafa Nyang'anyi akiongea machache kwenye sherehe hiyo ya Eid El Fitr iliyofanyika DMV huku akisisitiza umoja wa Watanzania ni kitu muhimu sana bila kujali itikadi zao, alisema amefurahi kukuta TAMCO aliyoianzisha wakati ule yeye akiwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani bado inaendelea kwa nguvu zote pia  Balozi Nyang;anyi alisisitiza Watanzania Waache majungu huku akisema kama mtu una jambo linakukera ni bora uliweke wazi kwani majungu hayajengi, pia aliendelea kwa kusema uwazi wa mapato na matumizi ni jambo kubwa kwenye jumuiya zetu lisipokuwa wazi Wanajumuiya hukosa imani na viongozi wao na hatima yake hufanya Jumuiya kulegalega na baadae kufa.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...