Jeshi la Polisi kanda maalum ya DAR ES SALAAM leo limefanikiwa kumkamata askari bandia akiwa amevaa Sare za Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamishina wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, DCP SULEIMAN KOVA amesema leo majira ya saa moja na nusu asubuhi wamefanikiwa kumkamata JAMES HUSSEIN mwenye umri wa miaka 45 mkazi wa KIMARA TANGI BOVU akiwa amevaa sare hizo huku akiendelea na utapeli wa kujifanya askari wa kitengo cha usalama barabarani.
Aidha Kamanda KOVA ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi mara wanapomtilia mashaka askari yeyote na pia kuwaomba wananchi  wasikubali kupigwa bao bali kuwataka askari kwenda nao kituo cha polisi pindi wanapokamatwa na makosa.
 Askari Bandia wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliyekamatwa leo mchana maeneo ya Kinyelezi Mnara,Tabata jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya sare zake mara baara ya kukamatwa. Askari huyu feki amefikishwa kwenye Kituo cha Polisi Stakishari ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
Afande feki huyo akiwa chini ya ulinzi wa Polisi mara baada ya kukamatwa akila vichwa maeneo ya Kinyerezi Mnara,Tabata jijini Dar es Salaam.
Afande feki huyo akiwa Kituo cha Polisi Stakishari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 36 mpaka sasa

  1. Ataishi vipi hapa mjini kila Mtu anajua yeye mwenyewe namna ya kutafuta rizikiYake si wa muachie tu!!!!

    ReplyDelete
  2. Sasa serikali ijiulize kwanini mtu achuke jukumu la kuwa police feki, kuna maslahi gani, ananufaika nini. Ni funzo gani lipo. Je jeshi la police linafanya kazi yake inavyo paswa au rushwa imeshamiri.

    ReplyDelete
  3. It's a personality disorder.USA huo ni ugonywa anahitaji dawa .

    ReplyDelete
  4. Hii inaonyesh jinsi Trafic Police walivyojaa rushwa mpaka inaonekana ni deal kujifanyisha Trafic Police ili kulamba hela za walalahoi!

    ReplyDelete
  5. Sura ya huyo Polic Feki siyo mpya ikiwa na magwanda hayo, nadhani sura hiyo imeshakuwa kwenye shughuli hiyo miaka mingi sasa ya za arobaini zilikuwa zimewadia. Huo ni uhujumu wa usalama barabarani unatakiwa kukomeshwa.

    ReplyDelete
  6. Jamaa kaharibu kuweka cheo kikubwa, angeweka Private asingestukiwa mapema hii Bongo we acha tu. Lakini jamaa ana uso wa Mbuzi

    Yaani wanatukamuaje siku hizi huna kosa anaomba Leseni anaenda kukaa chini ya Mti. Mpaka umpe chake ama akubambikie makosa LUKUKI.

    Tuanzae kuwarekodi kama Nigeria walivyofanya mpka jamaa akajiuzulu

    ReplyDelete
  7. Duuh, ee bana e hii kali! Ama kweli mjini shule!Jamaa kapiga hesabu weee kaona isiwe issue mbona wenyewe wanakula vichwa!!!ngoja na mimi nitege.Embu semeni wenyewe huyo apo akikukamata mpaka umng'amue ni feki lini? Walaahi nimenyoosha mikono.Naunga mkono jamaa kuna somo kaifundisha jamii, wamsamehe tu na kumuelekeza kufanya kazi kipato halali!!!

    ReplyDelete
  8. Je waliomkamata wamenawa mikono yao?Yesu angerudi akawajibu na kila mmoja angetoka njia yake.Tanzania kwa usawa wa utawala wa kizazi hiki hakuna wa kumcheka mwenzake

    ReplyDelete
  9. Katokelezea...

    ReplyDelete
  10. Huyo jamaa ni very creative inabidi apewe tuzo, ameangalia opportunity akaiona akaichukua.

    ReplyDelete
  11. Mwanadamu kwa sababu tu ya njaa anaweza kufanya lolote liwe baya/zuri bila kujali matokeo yake

    ReplyDelete
  12. Maisha magumu usipime,hivi tujiulize Uniform kapata wp? Inaonekana kuna trafic wa kweli kampa uniform maana haziuzwi mitumbani wala dukani,ila jamaa naye noma sana,hadi kofia na kifimbo? Duhhhhhh!

    ReplyDelete
  13. Tujiulize hayo magwanda ya police kayatoa wapi? Kama sio police haohao waliompa, au ni magwanda fake ameshona yeye! na kofia basi je kaipata wapi? na hicho kijambakoti kilichoandikwa police nacho kakitengeneza mwenyewe au kakwapua kwa askari?

    ReplyDelete
  14. Hizo sare Pia feki? Kwa muda gani alikua akifanya hiyo kazi yake ya kula vichwa. Maana kwa ukweli hapeleki mtu mbele ya sheria. Jamaa sasa atakufa maskini maana hiyo kazi kutwa si Chini ya laki. Akitoka kifungoni atafute mbinu nyingine maana mshahara atakayolipwa atauona kidogo. Ndio bongo kila mtu na akilii yake. Sheria ichukue mkondo wake akipatikana na kosa na adhabu iwe kubwa.

    ReplyDelete
  15. Mh sijui atakuwa anatokea mkoa wa mara yaani mzaliwa wa mara mana police wengi ni wazaliwa wa mara. Mh maajabu haya na lazima atakuwa anajua kuendesha gari mana bia hivyo makosa atayajuaje ya mwendesha gari? Au amekariri makosa wanayokamatwa nayo watu hivyo anarudia rudia tu! Duh bongo hiyo na opportunities zake.Kama vile namsikia anasema tutabanana hapa hapa mjini.

    ReplyDelete
  16. Sasa sisi madereva tutawajuaje orijino na feki. Orijino ukiwauliza kitambulisho umefungua kesi tunaogopa. Maana kesi itakua ya mambo mengi tu. Tusaidiane hapa maana maisha magumu unaangaika toka asubuhi jioni Jamaa feki anachukua kiulaini Kabisa.

    ReplyDelete
  17. Nimegundua alichokosea,uniform yake haina vifungo vyeusi vyenye nembo ya jeshi la polisi.Ina vifungo vya kugonga,vyeupe kama vya uniform za manesi,nadhani wataalamu wenzake walianzia hapo kumshtukia.Ila sasa kama mdau alivyosema,ukikamatwa utajuaje feki na wa ukweli,maana umeshatajiwa makosa kibao hata uniform utaangalia imekaaje wakati wanataka laki yao.Ila amejitahidi,ingawa kidogo atakuwa matatani.Labda wampeleke apike kwata wampe hiyo kazi maana anaipenda

    ReplyDelete
  18. ILA HUYO JAMAA KAMA ASIPOTAFUNA MANENO YATAGUNDULIKA MENGI.

    INAWEZEKANA HAKUPELEKA MGAO KWA WAZEE WAKAMCHOMA SASA NAMSHAURI AFANYIE KAZI ULE MSEMO WETU"UKIMWAGA MBOGA NAMI NAMWAGA UGALI"

    NDIO MAAJABU SABA YA DUNIA YATAONGEZEKA NA KUWA 8+

    ReplyDelete
  19. Huenda akawa ni mstaafi wa jeshi tena kwny kitengo hicho jicho cha trafick. Alishazoea kupiga bao, ss ameamua kujiajiri kwa kutumia uzoefu wake.

    ReplyDelete
  20. Huyu jamaa alishawahi kunkamata maeneo ya kigogo nikakomaa sikumpa kitu

    ReplyDelete
  21. Sasa ninyi mnataka mle rushwa peke yenu, na sisi tunataka.

    ReplyDelete
  22. tusilaumu tu pia mchango wake wa kukkomesha ajali za barabarani je na kudhibiti madereva feki pia ?

    Hongera wewe si feki bali umejitolea tu ulikuwa ufuate taratibu lakini pia wangekubania wewe unaitwa

    Voluntary worker au volunteer hongera lakini naona magwanda kidogo kama mazito hivi?

    ReplyDelete
  23. Jamaa ni noma kwanza ana uso wakibandigu huyo akikumata km hauko imara lazima utoe pesa ila jamaa creative sana wamuachie iyo ndo bongo dar es salaam ukizubaa unaachwa feri...

    ReplyDelete
  24. Huyu jamaa ni kibao, congrats kwa kutokuwa mwoga. He should either be taken to mental hospital or be given the highest honour of the country. The guy is creative.

    ReplyDelete
  25. Issue muhimu ni kwamba:

    1: Traffic police kuna opportunity pana zaidi ya kula rushwa- ndiyo maana hakujifanya, askari wa kawaida, mgambo wala mwanajeshi

    2: Huyu jamaa kakutwa na vifaa vyote muhimu- uniforms, notification forms, virungu etc. Ina, maana kuna mtu ambaye ni askari kampatia ili wagawane mpato

    3: Kila mara watu wanaposema jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kuna matatatizo hawazikilizwi- sasa evidence ndiyo hii. Je wapo wangapi wa aina hii Tanzania ahii

    ReplyDelete
  26. Kuna mdao aliandika orijino ukiwauliza kitambulisho anahisi umemdhalilisha. Imewahi kunitokea kwa mfanyakazi WA Tanesco.nilimwomva anionyeshe kitambulisho kosa. Aliondoka na kakataa line ktk nguzo nje. Sasa njoo ofisini nikuonyeshe kitambulisho. Ikabidi niende kumwona mkuu wake wa kazi. Nikamweleza Jamaa akaitwa akasema kweli amenikatia kwa sababu nilikua nimeunga umeme kwa njia ya uwizi. Nikageuziwa kibao hapa na pale zimenitoka. Tatizo letu kijicheo kidogo tuu tayari mtu anakua mungu mtu. Na Hapana pa kukimbilia polisi kwa sasa hivi ndio pa kupakimbia kabisa Hata kama umeonewa we malizana huko huko. Tunakwenda pabaya.

    ReplyDelete

  27. RUSHWA ILIYOKITHIRI! HICHO NI KIPIMO TOSHA CHA UADILIFU KWA WENYE KAZI HIYO. JE ASKARI USALAMA BARABARANI MMEONA MATUNDA YA UADILIFU WENU? NI AIBU TUPU DHAMBI NI LAZIMA IKUAIBISHE SIKU MOJA HAIKUACHI KAMA SI WEWE UTAAIBIKA NI KIZAZI CHAKO. WAZAZI TUFIKIRI MBELE TUSILISHE WATOTO DHAMBI ZETU HAWANA HATIA

    ReplyDelete

  28. Jamaa hana hatia hajashikwa akipokea rushwa wala nini kashikwa akijitolea (volunteer wa nguvu) apongezwe kwa kujitolea

    ReplyDelete
  29. mbona alipokamatwa alionekana kuzimia?

    Lkini wangemuacha tu, hicho ni koo kinaonyesha polisi walivyo.

    honera sana. k ova mwachie huyo amewapa fundisho. mapolisi wanakula rushwa

    ReplyDelete
  30. Jamani mawakili angaliueni namna ya kumwokoa huyu jamaa wa "ulinzi shirikishi". Amesaidia sana kudumisha usalama barabarani huko shamba ambako wengine hawataki kwenda. Kova mpe tano huyu jamaa.

    ReplyDelete
  31. Hongera jeshi la polisi kwa kufichua maovu

    ReplyDelete
  32. Polisi wameshindwa kazi wamejitia kuanzisha ulinzi shirikishi,sasa huu ulinzi una-extend mpaka usalama barabarani!nadhani utetezi wake uwe ni kwamba alikuwa kwenye jukumu la ulinzi shirikishi hususan kitengo cha usalama barabarani.

    ReplyDelete
  33. Genious. Why didn't I think of this money making scheme... Unfortunately he has to pay a price for impersonating a traffic police. However wampe community service - wasimfungie prison kwasababu amehighlight a big problem in the country that needs to be addressed. In the meantime we need to follow his every move -discretley- to see what techniques he invents next. Please ndugu Michuzi keep us updated on this case. Asante.

    ReplyDelete
  34. Hapo mwanzo nilipata hisia jamaa akipatikana na kosa afungwe. Baada ya kusoma baadhi ya comments nakubaliana nao, pamoja na jamaa kujifanya Askari ambalo ni kosa. Lakini hilo kosa ni muamsho mzuri kwa polisi serikali Jeshi mgambo na kadhalika wa kadhalika pamoja na CC waendesha magari. CC kutoa c kitu mtu unapenda. Nani anapenda kutoa alichokiangaikia ila ile kuangaishwa na hao polisi origin pundit ukakataa kutoa wanachotaka. Peleka Gari kituoni Achaa ufungua njoo kesho tukague Gari lako. Hapo sasa ni bora mkamaliziana kibongo. Utakapokubali. Kuacha siku ya pili utakuta vtu vingi vimenyofolewa. Its not worth it better finish for small amount of pay then lose much. Apewe adhabu ndogo kwani ametufumbua macho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...