Jeshi la Polisi kanda maalum ya DAR ES SALAAM leo limefanikiwa kumkamata askari bandia akiwa amevaa Sare za Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamishina wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, DCP SULEIMAN KOVA amesema leo majira ya saa moja na nusu asubuhi wamefanikiwa kumkamata JAMES HUSSEIN mwenye umri wa miaka 45 mkazi wa KIMARA TANGI BOVU akiwa amevaa sare hizo huku akiendelea na utapeli wa kujifanya askari wa kitengo cha usalama barabarani.
Aidha Kamanda KOVA ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi mara wanapomtilia mashaka askari yeyote na pia kuwaomba wananchi wasikubali kupigwa bao bali kuwataka askari kwenda nao kituo cha polisi pindi wanapokamatwa na makosa.
Askari Bandia wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliyekamatwa leo mchana maeneo ya Kinyelezi Mnara,Tabata jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya sare zake mara baara ya kukamatwa. Askari huyu feki amefikishwa kwenye Kituo cha Polisi Stakishari ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
Afande feki huyo akiwa chini ya ulinzi wa Polisi mara baada ya kukamatwa akila vichwa maeneo ya Kinyerezi Mnara,Tabata jijini Dar es Salaam.
Afande feki huyo akiwa Kituo cha Polisi Stakishari.
Ataishi vipi hapa mjini kila Mtu anajua yeye mwenyewe namna ya kutafuta rizikiYake si wa muachie tu!!!!
ReplyDeletenjaa tu
ReplyDeleteSasa serikali ijiulize kwanini mtu achuke jukumu la kuwa police feki, kuna maslahi gani, ananufaika nini. Ni funzo gani lipo. Je jeshi la police linafanya kazi yake inavyo paswa au rushwa imeshamiri.
ReplyDeleteNo comments.
DeleteIt's a personality disorder.USA huo ni ugonywa anahitaji dawa .
ReplyDeleteHii inaonyesh jinsi Trafic Police walivyojaa rushwa mpaka inaonekana ni deal kujifanyisha Trafic Police ili kulamba hela za walalahoi!
ReplyDeleteSura ya huyo Polic Feki siyo mpya ikiwa na magwanda hayo, nadhani sura hiyo imeshakuwa kwenye shughuli hiyo miaka mingi sasa ya za arobaini zilikuwa zimewadia. Huo ni uhujumu wa usalama barabarani unatakiwa kukomeshwa.
ReplyDeleteJamaa kaharibu kuweka cheo kikubwa, angeweka Private asingestukiwa mapema hii Bongo we acha tu. Lakini jamaa ana uso wa Mbuzi
ReplyDeleteYaani wanatukamuaje siku hizi huna kosa anaomba Leseni anaenda kukaa chini ya Mti. Mpaka umpe chake ama akubambikie makosa LUKUKI.
Tuanzae kuwarekodi kama Nigeria walivyofanya mpka jamaa akajiuzulu
Duuh, ee bana e hii kali! Ama kweli mjini shule!Jamaa kapiga hesabu weee kaona isiwe issue mbona wenyewe wanakula vichwa!!!ngoja na mimi nitege.Embu semeni wenyewe huyo apo akikukamata mpaka umng'amue ni feki lini? Walaahi nimenyoosha mikono.Naunga mkono jamaa kuna somo kaifundisha jamii, wamsamehe tu na kumuelekeza kufanya kazi kipato halali!!!
ReplyDeleteJe waliomkamata wamenawa mikono yao?Yesu angerudi akawajibu na kila mmoja angetoka njia yake.Tanzania kwa usawa wa utawala wa kizazi hiki hakuna wa kumcheka mwenzake
ReplyDeleteKatokelezea...
ReplyDeleteHuyo jamaa ni very creative inabidi apewe tuzo, ameangalia opportunity akaiona akaichukua.
ReplyDeleteMwanadamu kwa sababu tu ya njaa anaweza kufanya lolote liwe baya/zuri bila kujali matokeo yake
ReplyDeleteMaisha magumu usipime,hivi tujiulize Uniform kapata wp? Inaonekana kuna trafic wa kweli kampa uniform maana haziuzwi mitumbani wala dukani,ila jamaa naye noma sana,hadi kofia na kifimbo? Duhhhhhh!
ReplyDeleteTujiulize hayo magwanda ya police kayatoa wapi? Kama sio police haohao waliompa, au ni magwanda fake ameshona yeye! na kofia basi je kaipata wapi? na hicho kijambakoti kilichoandikwa police nacho kakitengeneza mwenyewe au kakwapua kwa askari?
ReplyDeleteHizo sare Pia feki? Kwa muda gani alikua akifanya hiyo kazi yake ya kula vichwa. Maana kwa ukweli hapeleki mtu mbele ya sheria. Jamaa sasa atakufa maskini maana hiyo kazi kutwa si Chini ya laki. Akitoka kifungoni atafute mbinu nyingine maana mshahara atakayolipwa atauona kidogo. Ndio bongo kila mtu na akilii yake. Sheria ichukue mkondo wake akipatikana na kosa na adhabu iwe kubwa.
ReplyDeleteMh sijui atakuwa anatokea mkoa wa mara yaani mzaliwa wa mara mana police wengi ni wazaliwa wa mara. Mh maajabu haya na lazima atakuwa anajua kuendesha gari mana bia hivyo makosa atayajuaje ya mwendesha gari? Au amekariri makosa wanayokamatwa nayo watu hivyo anarudia rudia tu! Duh bongo hiyo na opportunities zake.Kama vile namsikia anasema tutabanana hapa hapa mjini.
ReplyDeleteSasa sisi madereva tutawajuaje orijino na feki. Orijino ukiwauliza kitambulisho umefungua kesi tunaogopa. Maana kesi itakua ya mambo mengi tu. Tusaidiane hapa maana maisha magumu unaangaika toka asubuhi jioni Jamaa feki anachukua kiulaini Kabisa.
ReplyDeleteNimegundua alichokosea,uniform yake haina vifungo vyeusi vyenye nembo ya jeshi la polisi.Ina vifungo vya kugonga,vyeupe kama vya uniform za manesi,nadhani wataalamu wenzake walianzia hapo kumshtukia.Ila sasa kama mdau alivyosema,ukikamatwa utajuaje feki na wa ukweli,maana umeshatajiwa makosa kibao hata uniform utaangalia imekaaje wakati wanataka laki yao.Ila amejitahidi,ingawa kidogo atakuwa matatani.Labda wampeleke apike kwata wampe hiyo kazi maana anaipenda
ReplyDeleteILA HUYO JAMAA KAMA ASIPOTAFUNA MANENO YATAGUNDULIKA MENGI.
ReplyDeleteINAWEZEKANA HAKUPELEKA MGAO KWA WAZEE WAKAMCHOMA SASA NAMSHAURI AFANYIE KAZI ULE MSEMO WETU"UKIMWAGA MBOGA NAMI NAMWAGA UGALI"
NDIO MAAJABU SABA YA DUNIA YATAONGEZEKA NA KUWA 8+
Huenda akawa ni mstaafi wa jeshi tena kwny kitengo hicho jicho cha trafick. Alishazoea kupiga bao, ss ameamua kujiajiri kwa kutumia uzoefu wake.
ReplyDeleteHuyu jamaa alishawahi kunkamata maeneo ya kigogo nikakomaa sikumpa kitu
ReplyDeleteSasa ninyi mnataka mle rushwa peke yenu, na sisi tunataka.
ReplyDeletetusilaumu tu pia mchango wake wa kukkomesha ajali za barabarani je na kudhibiti madereva feki pia ?
ReplyDeleteHongera wewe si feki bali umejitolea tu ulikuwa ufuate taratibu lakini pia wangekubania wewe unaitwa
Voluntary worker au volunteer hongera lakini naona magwanda kidogo kama mazito hivi?
Jamaa ni noma kwanza ana uso wakibandigu huyo akikumata km hauko imara lazima utoe pesa ila jamaa creative sana wamuachie iyo ndo bongo dar es salaam ukizubaa unaachwa feri...
ReplyDeleteHuyu jamaa ni kibao, congrats kwa kutokuwa mwoga. He should either be taken to mental hospital or be given the highest honour of the country. The guy is creative.
ReplyDeleteIssue muhimu ni kwamba:
ReplyDelete1: Traffic police kuna opportunity pana zaidi ya kula rushwa- ndiyo maana hakujifanya, askari wa kawaida, mgambo wala mwanajeshi
2: Huyu jamaa kakutwa na vifaa vyote muhimu- uniforms, notification forms, virungu etc. Ina, maana kuna mtu ambaye ni askari kampatia ili wagawane mpato
3: Kila mara watu wanaposema jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kuna matatatizo hawazikilizwi- sasa evidence ndiyo hii. Je wapo wangapi wa aina hii Tanzania ahii
Kuna mdao aliandika orijino ukiwauliza kitambulisho anahisi umemdhalilisha. Imewahi kunitokea kwa mfanyakazi WA Tanesco.nilimwomva anionyeshe kitambulisho kosa. Aliondoka na kakataa line ktk nguzo nje. Sasa njoo ofisini nikuonyeshe kitambulisho. Ikabidi niende kumwona mkuu wake wa kazi. Nikamweleza Jamaa akaitwa akasema kweli amenikatia kwa sababu nilikua nimeunga umeme kwa njia ya uwizi. Nikageuziwa kibao hapa na pale zimenitoka. Tatizo letu kijicheo kidogo tuu tayari mtu anakua mungu mtu. Na Hapana pa kukimbilia polisi kwa sasa hivi ndio pa kupakimbia kabisa Hata kama umeonewa we malizana huko huko. Tunakwenda pabaya.
ReplyDelete
ReplyDeleteRUSHWA ILIYOKITHIRI! HICHO NI KIPIMO TOSHA CHA UADILIFU KWA WENYE KAZI HIYO. JE ASKARI USALAMA BARABARANI MMEONA MATUNDA YA UADILIFU WENU? NI AIBU TUPU DHAMBI NI LAZIMA IKUAIBISHE SIKU MOJA HAIKUACHI KAMA SI WEWE UTAAIBIKA NI KIZAZI CHAKO. WAZAZI TUFIKIRI MBELE TUSILISHE WATOTO DHAMBI ZETU HAWANA HATIA
ReplyDeleteJamaa hana hatia hajashikwa akipokea rushwa wala nini kashikwa akijitolea (volunteer wa nguvu) apongezwe kwa kujitolea
mbona alipokamatwa alionekana kuzimia?
ReplyDeleteLkini wangemuacha tu, hicho ni koo kinaonyesha polisi walivyo.
honera sana. k ova mwachie huyo amewapa fundisho. mapolisi wanakula rushwa
Jamani mawakili angaliueni namna ya kumwokoa huyu jamaa wa "ulinzi shirikishi". Amesaidia sana kudumisha usalama barabarani huko shamba ambako wengine hawataki kwenda. Kova mpe tano huyu jamaa.
ReplyDeleteHongera jeshi la polisi kwa kufichua maovu
ReplyDeletePolisi wameshindwa kazi wamejitia kuanzisha ulinzi shirikishi,sasa huu ulinzi una-extend mpaka usalama barabarani!nadhani utetezi wake uwe ni kwamba alikuwa kwenye jukumu la ulinzi shirikishi hususan kitengo cha usalama barabarani.
ReplyDeleteGenious. Why didn't I think of this money making scheme... Unfortunately he has to pay a price for impersonating a traffic police. However wampe community service - wasimfungie prison kwasababu amehighlight a big problem in the country that needs to be addressed. In the meantime we need to follow his every move -discretley- to see what techniques he invents next. Please ndugu Michuzi keep us updated on this case. Asante.
ReplyDeleteHapo mwanzo nilipata hisia jamaa akipatikana na kosa afungwe. Baada ya kusoma baadhi ya comments nakubaliana nao, pamoja na jamaa kujifanya Askari ambalo ni kosa. Lakini hilo kosa ni muamsho mzuri kwa polisi serikali Jeshi mgambo na kadhalika wa kadhalika pamoja na CC waendesha magari. CC kutoa c kitu mtu unapenda. Nani anapenda kutoa alichokiangaikia ila ile kuangaishwa na hao polisi origin pundit ukakataa kutoa wanachotaka. Peleka Gari kituoni Achaa ufungua njoo kesho tukague Gari lako. Hapo sasa ni bora mkamaliziana kibongo. Utakapokubali. Kuacha siku ya pili utakuta vtu vingi vimenyofolewa. Its not worth it better finish for small amount of pay then lose much. Apewe adhabu ndogo kwani ametufumbua macho.
ReplyDelete