Mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares (pichani Mbele),akiwa sambamba na baadhi ya Wadau waliojitokeza kuifanikisha hafla hiyo ya chakula cha mchana na watoto Yatima kutoka vituo vitatu,kushoto ni  Dada  Janet Sosthenes  Mwenda wa Ongea na Janet na wadau wengineo.
 Mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares akiongea na Watoto kutoka vituo Yatima,kabla ya kukata keki na kuwalisha.
Mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares akimlisha keki mmoja wa watoto waishio katika mazingira Magumu kutoka kituo cha Watoto yatima cha Vetenari Temeke.
 Watoto wakipakuliwa chakula safi kabisa.
Baadhi ya watoto kutoka vituo vya watoto Yatima,kituo cha Sifa Bunju,Zaidia Sinza pamoja na Vetenari Temeke,wamekutana leo mchana kwenye Fukwe ya Azura Beach Kawe kwa ajili ya kupata chakula cha pamoja na watoto wengine,huku michezo mbalimbali kama vile face painting,jumping castle,kuogelea,kuvuta kamba,mpira wa miguu,kucheza mziki n.k.Michezo hiyo iliyoandaliwa na Kids Event na mingineyo ilitawala na kuwaburudisha sana watoto.
Aidha mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares,amesema kuwa mkusanyiko huo unafanyika kufuatia zoezi zima la kukamilisha ule mpango ulioanza wa kuchangia vituo vya watoto yatima.

Pamoja na hafla hiyo pia Keki iliyoandaliwa na flying chefs  ilikatwa huku wasanii mbalimbali wakishiriki kwa pamoja,akiwemo Shilole,Snura,Quenn Darlin,Mwasiti na wengineo.Janet Sosthenes  Mwenda wa Ongea na Janet na Wasanii wengine walijitolea kuwahudumia na kuwaangalia watoto.
Dina Marios anawashukuru watu wote walioshiriki kuchangia vituo hivyo.Wadau wa blog yake www.dinamarios.blogspot.com wasikilizaji wa leo tena ya clouds fm na wote walioguswa. Mpango huo utaendelea siku nyingine tena maana ni endelevu.
PICHA ZAIDI INGIA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Money well spent, God luv you all!!! and keep up the good work.

    ReplyDelete
  2. Hongera Dina kwa Uenezi huo!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...