Mratibu
wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares (pichani Mbele),akiwa
sambamba na baadhi ya Wadau waliojitokeza kuifanikisha hafla hiyo ya
chakula cha mchana na watoto Yatima kutoka vituo vitatu,kushoto ni
Dada Janet Sosthenes Mwenda wa Ongea na Janet na wadau wengineo.
Mratibu
wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares akiongea na Watoto
kutoka vituo Yatima,kabla ya kukata keki na kuwalisha.
Mratibu
wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares akimlisha keki mmoja
wa watoto waishio katika mazingira Magumu kutoka kituo cha Watoto yatima
cha Vetenari Temeke.


Watoto wakipakuliwa chakula safi kabisa.
Baadhi
ya watoto kutoka vituo vya watoto Yatima,kituo cha Sifa Bunju,Zaidia
Sinza pamoja na Vetenari Temeke,wamekutana leo mchana kwenye Fukwe ya
Azura Beach Kawe kwa ajili ya kupata chakula cha pamoja na watoto
wengine,huku michezo mbalimbali kama vile face painting,jumping castle,kuogelea,kuvuta kamba,mpira wa miguu,kucheza mziki n.k.Michezo hiyo iliyoandaliwa na Kids Event na mingineyo ilitawala na kuwaburudisha sana watoto.
Aidha
mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares,amesema kuwa
mkusanyiko huo unafanyika kufuatia zoezi zima la kukamilisha ule mpango
ulioanza wa kuchangia vituo vya watoto yatima.
Pamoja
na hafla hiyo pia Keki iliyoandaliwa na flying chefs ilikatwa huku
wasanii mbalimbali wakishiriki kwa pamoja,akiwemo Shilole,Snura,Quenn
Darlin,Mwasiti na wengineo.Janet Sosthenes Mwenda wa Ongea na Janet na Wasanii wengine walijitolea kuwahudumia na kuwaangalia watoto.
Dina
Marios anawashukuru watu wote walioshiriki kuchangia vituo hivyo.Wadau
wa blog yake www.dinamarios.blogspot.com wasikilizaji wa leo tena ya
clouds fm na wote walioguswa. Mpango huo utaendelea siku nyingine tena maana ni endelevu.
PICHA ZAIDI INGIA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM
Money well spent, God luv you all!!! and keep up the good work.
ReplyDeleteHongera Dina kwa Uenezi huo!!!
ReplyDelete