Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Ndugu Hassan Mtenga, (uu akipokea kadi ya CHADEMA toka kwa ndugu Grace Mbowe na chini akimkabidhi kadi ya CCM, Ndugu Grace Mbowe, baada ya kutoka CHADEMA kwa kile alichodai hakuna jambo jipya.
DADA wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ndugu Grace Mbowe, amejiunga na Chama Cha Mapinduzi ( CCM) akitokea Chadema, kwa kile alichodai haoni jambo jipya katika chama hicho.
Grace amesema amehama kutokana na kuwepo propaganda zisizotekelezeka. Hata hivyo, amesisitiza kwamba kuwepo kwake katika Chadema, siyo kwa sababu ya familia. Alikabidhi kadi hiyo jana kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Hai. Alisema itikadi za kisiasa, zisihusishe masuala ya kifamilia, kwani upendo wao uko pale pale.
Alisema kilichomfanya kujiunga na chama hicho ni utashi wake. Alidai CHADEMA wanafanya propaganda za 
kuwadanganya wananchi.
Alisema itikadi za chama, haziwezi kuingilia masuala ya kifamilia, hivyo kwake siyo ajabu kuondoka CHADEMA, kwani kila mtu ana utashi wake wa kisiasa.
“Nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushawishiwa na mtu, ndio maana nimetoka Dar es Salaam kuja Hai kwa ajili ya kurejesha kadi ya CHADEMA na kujiunga na CCM, suala la itikadi lisihusishe masuala ya kifamilia kwani upendo wetu upo palepale,”alisema Mbowe.
Alisema, “kuwapo kwangu CHADEMA siyo kwa sababu ya familia, hivyo hakuna wa kunizuia, natoka kwa utashi wangu, na tutaendelea kuheshimiana na mdogo wangu Freeman Mbowe katika masuala ya kifamilia.”
“Freeman Mbowe ni mdogo wangu wa kuzaliwa kabisa, hakunishawishi kuingia CHADEMA, hivyo sioni haja ya kuendelea kubaki huku wakati sioni jambo jipya, mimi tangu naifahamu CCM iko vile vile, bali propaganda za upinzani ndizo zinawalaghai wananchi,” alisema.
Aliviasa vyama vya siasa, kuwa sasa umefika wakati wa kuacha malumbano na maandamano ya itikadi, yasiyokuwa na faida yoyote, badala yake huu ni muda wa kujenga nchi kwa ushirikiano.
Awali, akipokea kadi ya CHADEMA, Katibu wa CCM Wilaya ya Hai, Hassan Mtenga alisema alichokifanya Grace ni uamuzi wa busara, baada ya kutazama Chadema ilipo na inapokwenda.
Alisema wimbi la wanachama wa Chadema kurudisha kadi na kujiunga na CCM, limekuwa kubwa wilayani Hai. Alisema tangu Januari hadi sasa amepokea wanachama 530.
Mtenga aliwataka wananchi kutambua kwamba Jimbo la Hai, siyo kitovu cha upinzani bali CHADEMA ni chama kilichotoa upinzani kwa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2010. Alisema hali hiyo, ilitokana na makundi ya CCM.
Alisema kwa sasa watu asitarajie tena suala hilo kutokea. 
CHANZO: HABARILEO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Nadhani huyu Ana-igiza tu na baadae atarudi nyumbani kwao alikotoka.Na zaidi ya kuongeza idadi tu,Sibiu amekuja kuongeza thamani gani.Acha tusubiri tuone mwisho wa Cinema hii

    ReplyDelete
  2. Tatizo la vyama nchini mwetu ni kwamba havina nadharia yoyote. Si wajamaa , si wahafidhina ,si mabepari ,siwakomunist ,ni makundi tu ya wapepeta midomo basi. Sasa dada yetu Mbowe unaingia ccm ukidai chadema haina jipya, umeona jipya gani ccm? Sioni tofauti kati ya ccm na chadema.

    ReplyDelete
  3. ni kama kusema wacha niwe mlokole! tehee! amesikia kuitwa na ccm. Siasa na ile ile dada Mbowe. jaribu jaribu tu njoo kwetu wana NCCR mageuzi! hapo hutageuka kamwe!

    ReplyDelete
  4. Very wise and intelligent woman!!!But how can she sustain in her every day life? Definitely the brother's money will immediately 'evaporate'!!!
    I think she'd to think thrice before taking this hard decision.

    ReplyDelete
  5. Huu ni unafiki Grace. Lazima una hila. Kwa nini usikabidhi hiyo kadi ya Chadema kimya kimya kama ulivyo ichukua Kimnya? Tangu umekuwa mwanachama wa chadema mbona ulikuwa hujatueleza tija, umahiri uliyotuletea sisi wana nchi ukiwa mwana mapunduzi? Mwenye msimamo madhubuti haondoki, anawezesha mabadiliko pale alipo. Hatangi-tangi kama ilivyo desturi ya baadhi ya watu!!!

    ReplyDelete
  6. JAMANI MSIDANGANYIKE HUU NI UGOMVI WA WANANDUGU TU!! HAKUNA CCM WALA CHADEMA. HUYU DADA ANATAFUTA UMAARUFU TU.

    ReplyDelete
  7. It is all a circus, let us see on how it ends. Probably a photo opportunity, she has been always upstaged by the brother.

    ReplyDelete
  8. Ametumia akili sana huyu dada!

    Mdau wa kwanza kwa taarifa yako baba yao akina Freeman Mbowe na huyu Anastasia Mbowe (MZEE MBOWE) ni KADA MKUBWA SANA WA CHAMA CHA MAPUINDUZI !!!

    Acheni ubishi maana yake huyo dad ndio amerudi kwao sasa tofauti na unavyodai atarejea CHD!

    Bado Freeman Mbowe sasa kuhamia CCM!

    ReplyDelete
  9. Freeman Mbowe naye anarudi CCM kabla ya Ucdhaguzi Mkuu 2015!

    Mnabisha?

    ReplyDelete
  10. Ametumia akili asana dada Anastasia Mbowe kuelewa ya kuwa CDM hawa chao!

    ReplyDelete
  11. Mdaun wa kwanza Samson Cotton Agenda:

    Dada Grace Mbowe amesoma vyema Alama za Nyakati na amegundua ya kuwa katika Chadema hakuna Siasa bali ubabaishaji tu.

    Hebu angalia Waheshimiwa kla kukicha ni wao kuvunja Sheria na kusakwa na Polisi na kuburuzwa na Mahakama badala ya kupigania mambo yenye tija Kisiasa kwa ajili ya Umma.

    Chadema KWISHNEY !

    ReplyDelete
  12. Mnaweza kuzaliwa wengi wachache wakawa na kili.

    Sio wote, tena cha ajabu yule anayeonekana ni majanja asiwe na akili kama mwingine asiye tegemewa kabisa.

    Dada Grace Mbowe ana akili sana, amepiga picha akaona hapana akaingia CCM!

    ReplyDelete
  13. Dada Grace Mbowe amegundua ya kuwa CDM kuingia Ikulu labda jua LICHOMOZE MAGHARIBI NA KUZAMA MASHARIKI!

    Akaona ahamie CCM!

    ReplyDelete
  14. dada Mbowe amesema vema 'mimi tangu naifahamu CCM iko vilevile'

    ReplyDelete
  15. She is wise women I know her and if she say that then its real

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...