Globu ya Jamii ina furaha na fahari kutangaza kwamba hatimaye wazazi wa mtoto wa kike Manka wamepatikana na tayari wamemchukua binti yao tokea jana usiku.
Manka, mwenye umri kati ya miaka 3-4 ambaye jana jioni tulimtangaza kuwa ameokotwa maeneo ya Upanga jijini Dar es salaam na kuhifadhiwa kituo kidogo cha Polisi cha Salender, ameungana na wazazi wake ambao waliiona taarifa hii mara moja.
Msamaria mwema aliyetuma habari hii anasema amefurahi sana wazazi wa Manka kupatikana kwani kama mzazi alijihisi vibaya sana kuona mtoto kapotea. Anawashukuru pia askari wa kituo cha Salender kwa kufanikisha hilo. Anamtakia Manka maisha mema na ya fanaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Aise shukran sana Ankal, you are the best of all .... inabidi upewe kikombe

    ReplyDelete
  2. What a shame!!! uzembe wa hali ya juuuu

    ReplyDelete
  3. Alipotea ktk mazingira yapi?

    ReplyDelete
  4. Shukrani kwa bloggi ya jamii na kituo cha usalama mtoto wetu Manka kaungana na wazazi kwa juhudi zenu
    za kujenga taifa pia kwa wadau wote wa humu ndani tumeonyesha moyo wa upendo kwa jamii hata hivyo ni kweli wadau zidi ya bloggi ya jamii tunategemea dogojr wa bloggi ya "Mtaa Kwa Mtaa" kujituma mitaani zaidi kwa kuwaweka hadharani watoto wa mitaani kama wadau wasemavyo wapo wengi maeneo ya fire kuwakumbusha wahusika wa asasi za "malezi ya watoto yatima" kupitia ngazi za serikali kuwaondoa watoto mitaani hata kama wazazi wanahusika wapate malezi na elimu ya msingi na ya kati kama watoto wengine.

    TANZANIA KILA MTOTO ANAYO HAKI YA MALEZI,ELIMU YA MSINGI NA YA KATI
    Mikidadi-Denmark

    ReplyDelete
  5. msemaji anayesema ni uzembe hajafafanua. Sijui uzembe wa nani! Mimi kwa upande wangu , huyu mtoto anapaswa kuelekezwa kuwa anatulia mahali kunakostahili.

    Mtoto kupotea ni tatizo la mtoto mwenyewe si uzembe wa wazazi.

    Kwanza ilibidi achapwe viboko.

    ReplyDelete
  6. Anonymous number 2 hauna mtoto, huwajui watoto wewe! Siku yakikukuta ndo utajua kuwa ni shame au vp.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...