1
Mtoto Ashura Mustapha (7) mkazi wa Mwandege, wilayani Mkuranga, Pwani anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi tangu akiwa na mwaka mmoja.
Akizungumza na mwandishi wetu, baba mzazi wa mtoto huyo, Mustapha Makombe alisema: “Mwanangu anateseka sana jamani, ugonjwa ulianza kama malengelenge akiwa na umri wa mwaka mmoja tukawa tunakwenda hospitali ndogondogo lakini baadaye tukaamua kumpeleka Muhimbili ambapo tulipewa barua ya kutuelekeza kwenda CCBRT, kule ndipo wakagundua mwanangu ana kansa ya ngozi steji ya nne.
2
“Baada ya kuhangaika katika hospitali nyingi bila mafanikio, nikaamua kwenda Hospitali ya Regency (Dar) kuomba msaada wa kwenda kutibiwa India.
“Pale waliniambia nichangie shilingi milioni moja na laki tano kwa ajili ya tiketi na viza ili mwanangu akatibiwe India, hizo hela mimi sina. Naomba Watanzania mnisaidie hata kwa fedha za mitandao kwa namba 0769 517765 ili niweze kumpeleka mwanangu India akatibiwe,” alisema baba mzazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Jamani Mungu amuepushe apone haraka hayo maradhi. Duuuu mimi nilifikiri kansa ya ngzi ni kwa watu weupe tu kwa sababu ya ubora mdogo wa ngozi zao kumbe hata kwetu imeingia?

    ReplyDelete
  2. Mtoto Ashura atapona kwa Uwezo na Upendo wa Yesu Kristu. Amini na Mpeleke penye maombi na Yesu atafanya miujiza ya uponyaji. Hivi punde nimemuweka mtoto katika maombi. Yangu hayatoshi na ni dhaifu. Baba na Mtoto Amini Christu omba, ombewa na utapona.

    ReplyDelete
  3. Serikali yetu sikivu imesikia kilio hiki.

    ReplyDelete
  4. AMPELEKE KWA TB JOSHUA MBONA HARAKA TU ANAPONA

    ReplyDelete
  5. Tanzania kuna matatizo sana. Such kids are supposed to be picked up by the system itself and taken care of. Mfumo unaofanya kazi sawa hauhitaji mtu ashikwe mkono na Waziri ndio apelekwe nchi ya nje kutibiwa. Kunatakiwa kuwe na medical criteria ama indications tu za mtu kwenda kutibiwa nje na si kufahamiana na fulani. We live in a sad system. System ingekuwa inafanya kazi basi matangazo kama haya tusingekuwa tunayaona.

    ReplyDelete
  6. Inasikitisha. Michuzi usilitoe mapema hili Tangazo ili watu wengi waguswe na hamsini hamsini tutakazotoa ziweze kumsaidia huyu binti.

    Mungu atakuzidishia.

    sesophy

    ReplyDelete
  7. nakubaliana na mchangiaji wa mwisho , na kwa kuongezea haya mambo ya kufuturisha watu walioshiba na wenye uwezo wao kiuchumi kama inavyofanyika hivi sasa kwa kutumia mamilioni ya fedha , ni bora mara isio na idadi hizo fedha wakapelekwa wagonjwa kama hawa kwa matibabu.Sytem yetu kweli ni mbovu kila kitu kujuana tu. pengine hata hili tangazo kuwekwa humu ni kwa kujuana, hee jamani tutamjibu nini Mungu?

    ReplyDelete
  8. Pole sana Ashura. Tunakuombea upate nafuu mapema. Mtoto mzuri kama wewe lakini serikali yetu ya mafisadi haijui kwamba wewe na watoto wenzako mlitakiwa kupewa kipao mbele kiafya, elimu na malazi.

    ReplyDelete
  9. Wengi wamechangia kwa kadiri ya kuguswa kwao na suala hili, nami pia kwa kuguswa kwa suala hili nimeamua nisiangalie picha tu bila ya kusema chochote wenda kikawa na manufaa iwe kwa huyu mtoto au hata wengine ambao naamini bado hawajapata nafasi ya kuwekwa hapa.Mimi nataka kuzungumzia mfumo unaotumika ktk hospitali zenu wenda ukawa si sahihi, na hili laweza ikawa ni sababu ya kutokujua au kujitia kujua sana kwa wataalam wetu,nafafanua:mara nyingi mgonjwa anapofika hospitali na kuonwa na hao waganga wetu hasa kule ktk hatua za mwanzo hapa nakusudia hospitali ndogo ambazo ndio kituo cha kwanza,huwa wanapoteza mda mwingi wa mgonjwa japo ipo wazi kwamba, kumtibu ama kumrifaa mgonjwa yote ni misaada yenye manuafaa kwa mgonjwa(kuwahi kabla ugonjwa hauja sambaa,kuokoa fedha,muda na mengineyo),kwa baadhi ya wataalam wetu hili la kumrifaa mgonjwa ni kama fedheha kwao,yaani inaonekana kama umeshindwa kumtibu hivyo hujaribu kupoteza muda mwingi japo anajua kwamba hana msaada kwa mgonjwa,kwa ufahamu wangu,kuna mifumo mitano ambayo mwanadamu anayo na magonjwa yamegawanywa kwa kufuata mifumo hiyo(Uzazi na mkojo,moyo na mishipa ya damu,ngozi,mfumo wa fahamu na mfumo wa chakula),inafahamika kwamba baadhi ya hospitali nyingi ninazozizungumzia hapa hazina wataalam wa haya magonjwa, waliokuwepo ni wale general physician au wale wa kiwango cha diploma kulingana na hospitali ipi umefikia/pokewa,hawa wanafahamu fika ni mfumo gani kati ya hiyo mitano niliyoitaja umeathirika na kwa kutambua kwao ni msaada tosha iwapo wanafahamu hakuna mtaalam(specialist)hapo walipo hivyo ni rahisi kuokoa muda na kumpeleka mgonjwa kule anapostahili.Mara nyingi nimeona wanandugu wenyewe ndio huwa wanaomba wapewe ruhusa kwenda mbele kwakua hawaoni nafuu kwa mgonjwa wao,Kwa mujibu wa taarifa hii ya huyu mtoto inasema ameanza kuugua aikiwa na mwaka mmoja na leo hii ana miaka saba, ninaamini amepita sehemu nyingi zaidi ya hizo alizozitaja na tuliowengi tunafahamu wapi ilipo hospitali maalum ya kansa lakini hata ktk hii taarifa haioneshi kama aliwahi fika huko.Kwa wanaofahamu stages and grades za kansa wanajua ni nini stage4.Nawasihi chondechonde madaktari/wataalam wetu wa ngazi za mwanzo si ujinga na si fedheha kumpeleka mbele mgonjwa pindi ukiona tatizo ni zaidi uwezo wako binafsi au hospitali ulipo kwa kufanya hivyo,tutapunguza vifo vingi,tutaokoa rasili mali,fedha, muda na hata kujijengea heshima binafsi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...