Balozi wa Tanzania Ufaransa, Mhe.
Begum Taj, akiwa na Lelo Elvis Munis, kijana ambae anaendesha baiskeli yake
kutoka Chile, iliyoko Marekani Latini, kurudi nyumbani Tanzania, katika juhudi
za kukusanya fedha za ada ya kuwezesha vijana 10 kusomea shahada za kuhifadhi
mazingira na maendeleo endelevu katika vyuo vya elimu ya juu.
Leo Lelo alikatiza safari yake kidogo na kwenda
kusalimia Ubalozini Paris. Vile vile alikaribishwa kwenye kituo cha televisheni
cha France 24 na kituo cha redio cha Radio France Internationale (RFI) ambako
alimhojiwa juu ya safari na malengo yake.
Mahojiano aliyofanya France 24 yanaweza kuonekana hapa http://www.france24.com/en/20130827-2013-08-27-2146-africa-news.
Kutoka Paris, Lelo ataelekea kusini
mwa Ufaransa kisha atavuka mpaka kuelekea Spain na Ureno. Kwa habari zaidi juu
ya safari ya Lelo na kuweza kuchangia mradi huu wa kusomesha vijana wa
Tanzania, tafadhali nendeni kwenye Tovuti yake iliyopo kwenye anwani hii: www.chiletokili.com.



Safi sana, ni wazo zuri.
ReplyDelete