Balozi wa Tanzania Ufaransa, Mhe. Begum Taj, akiwa na Lelo Elvis Munis, kijana ambae anaendesha baiskeli yake kutoka Chile, iliyoko Marekani Latini, kurudi nyumbani Tanzania, katika juhudi za kukusanya fedha za ada ya kuwezesha vijana 10 kusomea shahada za kuhifadhi mazingira na maendeleo endelevu katika vyuo vya elimu ya juu.  
Leo Lelo alikatiza safari yake kidogo na kwenda kusalimia Ubalozini Paris. Vile vile alikaribishwa kwenye kituo cha televisheni cha France 24 na kituo cha redio cha Radio France Internationale (RFI) ambako alimhojiwa juu ya safari na malengo yake.  Mahojiano aliyofanya France 24 yanaweza kuonekana hapa http://www.france24.com/en/20130827-2013-08-27-2146-africa-news.

Kutoka Paris, Lelo ataelekea kusini mwa Ufaransa kisha atavuka mpaka kuelekea Spain na Ureno. Kwa habari zaidi juu ya safari ya Lelo na kuweza kuchangia mradi huu wa kusomesha vijana wa Tanzania, tafadhali nendeni kwenye Tovuti yake iliyopo kwenye anwani hii:    www.chiletokili.com.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...