Kampuni ya Neema Herbalist kwa kushirikiana na Taasisi ya Flatbelly Tanzania ama FlabelTa imejipanga kutengeneza mamia ya fursa za ajira kwa vijana wasio na ajira wanaoishi kwenye kata mbalimbali za jijini Dar Es salaam. 
 Fursa hizo za ajira zitatengenezwa kupitia Mradi wa Flatbelly Project ambao umelenga katika kuwahamasisha wananchi wa kada mbalimbali jijini Dar es salaam,kuondokana na tatizo la vitambi,unene na/ama uzito ulio kithiri kwa kutumia dawa za asili, vyakula lishe ama tibalishe. Mradi huu utawanufaisha vijana watano kutoka katika kila kata ya jiji la Dar Es salaam ambao watapatiwa mafunzo maalumu ya yatakayo wajengea uwezo wa kufanya kazi katika mradi huu. Mafunzo watakayo patiwa vijana hawa ni pamoja na NAMNA YA KUANDAA LISHE ( DIET )MAALUMU KWA WATU WENYE MATATIZO YA VITAMBI,UNENE & UZITO MKUBWA KUPITA KIASI, pamoja na JINSI YA KUKUSANYA TAARIFA ZA WATU WENYE MATATIZO YA VITAMBI, UNENE NA UZITO MKUBWA WALIOPO KATIKA MAENEO MBALIMBALI KAMA VILE MAOFISINI NA MAJUMBANI. 
Mafunzo yatafanyika kwa muda wa wiki moja kuanzia tarehe 23 Septemba 2013 hadi tarehe 28 Septemba 2013. Baada ya mafunzo, wahitimu watapangiwa vituo vya kazi katika kata mbalimbali za jijini Dar Es salaam ambapo watapewa jukumu la kukusanya taarifa za watu wenye matatizo ya vitambi,unene na uzito kupita kiasi na kuwa andikisha katika program maalumu ya kuwasaidia kuondokana na tatizo la vitambi, unene na uzito mkubwa kwa kutumia dawa za asili, vyakula dawa na tibalishe kazi ambayo wataianza rasmi mnamo tarehe 01 OKTOBA 2013. 
Majukumu mengine watakayo patiwa vijana hawa ni pamoja na kuandaa na kusimamia semina mbalimbali kuhusu masuala ya umuhimu wa tibalishe kwa watu mbalimbali kama vile akina mama wa majumbani na wanawake wajasiriamali wanao jihusisha na biashara ya upishi wa vyakula vya aina mbalimbali.
 Katika kuhakikisha kuwa vijana watakao patiwa mafunzo haya wanakuwa na uwezo wa kufanya kazi kwenye mradi huu kwa ufanisi mkubwa, taasisi kwa kushirikiana na kampuni ya Neema Herbalist itakuwa ikitoa warsha na semina elekezi za mara kwa mara kwa vijana hawa katika kipindi chote cha mwaka mmoja ambacho watakuwa wanafanya kazi chini ya mradi huu. 
Mradi huu hautaishia jijini Dar Es salaam pekee, kwani baada ya vijana waliopo jijini Dar Es salaam kuanza kazi ,mradi utaelekea katika mikoa mingine ya Tanzania bara katika utaratibu na ratiba itakayo tangazwa katika blogu yetu na vyombo mbalimbali vya habari mwishoni mwa mwezi Septemba au mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2013. 
Sifa za kujiunga na mafunzo haya ni kuwa raia wa Tanzania mwenye elimu ya kuanzia kidato cha nne, sita na kuendelea, uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha kwa lugha za Kiswahili na kiingereza, uwezo wa kujieleza, umaridadi kujituma na kuwa tayari kufanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja katika mradi huu kama Mshauri/Muelimishaji kuhusu masuala ya tibalishe. 
 KWA TAARIFA ZAIDI KUHUSU UTARATIBU WA KUJIUNGA NA MAFUNZO HAYA, TAFADHALI TEMBELEA 
http://www.neemaherbalist.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hivi tofauti ya unene kitambi na uzito kupita kiasi lol

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...