Kampuni ya Neema Herbalist kwa kushirikiana na Taasisi ya
Flatbelly Tanzania ama FlabelTa imejipanga kutengeneza mamia ya
fursa za ajira kwa vijana wasio na ajira wanaoishi kwenye
kata mbalimbali za jijini Dar Es salaam.
Fursa hizo za
ajira zitatengenezwa kupitia Mradi wa Flatbelly Project ambao
umelenga katika kuwahamasisha wananchi wa kada mbalimbali jijini
Dar es salaam,kuondokana na tatizo la vitambi,unene na/ama
uzito ulio kithiri kwa kutumia dawa za asili, vyakula lishe
ama tibalishe.
Mradi huu utawanufaisha vijana watano kutoka katika kila kata
ya jiji la Dar Es salaam ambao watapatiwa mafunzo maalumu
ya yatakayo wajengea uwezo wa kufanya kazi katika mradi huu.
Mafunzo watakayo patiwa vijana hawa ni pamoja na NAMNA YA
KUANDAA LISHE ( DIET )MAALUMU KWA WATU WENYE MATATIZO YA
VITAMBI,UNENE & UZITO MKUBWA KUPITA KIASI, pamoja na JINSI YA
KUKUSANYA TAARIFA ZA WATU WENYE MATATIZO YA VITAMBI, UNENE NA
UZITO MKUBWA WALIOPO KATIKA MAENEO MBALIMBALI KAMA VILE
MAOFISINI NA MAJUMBANI.
Mafunzo yatafanyika kwa muda wa wiki moja kuanzia tarehe 23
Septemba 2013 hadi tarehe 28 Septemba 2013. Baada ya mafunzo,
wahitimu watapangiwa vituo vya kazi katika kata mbalimbali za
jijini Dar Es salaam ambapo watapewa jukumu la kukusanya
taarifa za watu wenye matatizo ya vitambi,unene na uzito
kupita kiasi na kuwa andikisha katika program maalumu ya
kuwasaidia kuondokana na tatizo la vitambi, unene na uzito
mkubwa kwa kutumia dawa za asili, vyakula dawa na tibalishe
kazi ambayo wataianza rasmi mnamo tarehe 01 OKTOBA 2013.
Majukumu mengine watakayo patiwa vijana hawa ni pamoja na
kuandaa na kusimamia semina mbalimbali kuhusu masuala ya
umuhimu wa tibalishe kwa watu mbalimbali kama vile akina
mama wa majumbani na wanawake wajasiriamali wanao jihusisha na
biashara ya upishi wa vyakula vya aina mbalimbali.
Katika
kuhakikisha kuwa vijana watakao patiwa mafunzo haya wanakuwa
na uwezo wa kufanya kazi kwenye mradi huu kwa ufanisi
mkubwa, taasisi kwa kushirikiana na kampuni ya Neema Herbalist
itakuwa ikitoa warsha na semina elekezi za mara kwa mara kwa
vijana hawa katika kipindi chote cha mwaka mmoja ambacho
watakuwa wanafanya kazi chini ya mradi huu.
Mradi huu hautaishia jijini Dar Es salaam pekee, kwani baada
ya vijana waliopo jijini Dar Es salaam kuanza kazi ,mradi
utaelekea katika mikoa mingine ya Tanzania bara katika
utaratibu na ratiba itakayo tangazwa katika blogu yetu na
vyombo mbalimbali vya habari mwishoni mwa mwezi Septemba au
mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2013.
Sifa za kujiunga na mafunzo haya ni kuwa raia wa Tanzania
mwenye elimu ya kuanzia kidato cha nne, sita na kuendelea,
uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha kwa lugha za Kiswahili na
kiingereza, uwezo wa kujieleza, umaridadi kujituma na kuwa
tayari kufanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja katika mradi huu
kama Mshauri/Muelimishaji kuhusu masuala ya tibalishe.
KWA TAARIFA ZAIDI KUHUSU UTARATIBU WA KUJIUNGA NA MAFUNZO
HAYA, TAFADHALI TEMBELEA
http://www.neemaherbalist.blogspot.com


hivi tofauti ya unene kitambi na uzito kupita kiasi lol
ReplyDelete