Naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge akipata maelezo kuhusu miradi
ya maji wilayani Same kutoka kwa mhandisi wa maji wilaya ya Same Musa
Msangi.
Naibu waziri wa maji Dk Binilithi Mahenge akiangalia moja ya vilula
vilivyojengwa katika kijiji cha Miombo wilayani Same.
Naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge akiongea na wananchi wa
kijiji cha Miombo wilayani Same ambao hata hivyo walidai tangu uhuru
hawakuwahi kumuona waziri aliyefika katika kijiji hicho.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mteke wilayani Same Samson Kimbuta akiongea
wakati wa mkutano mdogo wa wananchi wa kijiji hicho na naibu waziri wa
maji Dk Binilith Mahenge aliyetembelea kijiji hicho.
Diwani wa kata ya Mhezi katika kijiji cha Mteke wilayani Same Allen
Mbaga kiongea wakati wa mkutano mdogo wa wananchi wa kijiji hicho na
naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge aliyetembelea kijiji hicho.
Dk Binilith Mahenge akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mteke wilayani
Same wakati wa ziara yake kutembelea miradi ya maji katika wilaya
hiyo.
Picha na Dixon Busagaga waglobu ya jamii Moshi.


Eti hawajawahi kumuona waziri toka uhuru kuja kututembelea, mie Bibi yangu kule kijijini upareni bado anazani nyerere yupo na bado ni rais.kazi kweli kweli.
ReplyDeleteKwenye mradi wa maji wamepanda mikaratusi? sasa hapo si balaa maana hii miti inafyonza sana maji, waing'oe na wapande miti ya asili hasa mikuyu
ReplyDeleteDah! Nimepakumbuka sana kwa babu yangu Bombo Mjema!
ReplyDeleteOmbe thimanya, nnetonga rini ambu nethina Green card. Yeeuwii nnefwia he ili ithanga la Obama
Kumbe Upareni kuna migomba na ukijani? mie nafikiri ni kama jangwani tu!
ReplyDeleteMdau Mwathu hao wanga wanishingha hoi! Hunduka kaa shingha vurundu. Unefwia nyika kididi. Ohoooo
ReplyDelete