Familia ya Bwana Isaac Kalumuna wa Mbezi Beach Dar Es Salaam anatangaza kifo cha mkewe Annastazia Rwegasiraa Kalumuna (pichani) kilichotokea Ijumaa 23 Agosti 2013 katika Hospitali ya Massana, Mbezi.
Mazishi yatafanyika Alhamisi wiki hii, Agosti 29, mwaka huu, 2013 katika Kijiji cha Buganda, Kamachumu, Muleba, Mkoani Kagera.
Mwili utaagwa Leo Jumanne 27 Agosti nyumbani kwa marehemu, Art gallery Mbezi beach.
Kwa tangazo hili, habari ziwafakie ndugu, jamaa na marafiki.
"Bwana ametoa Bwana ametwaa"


Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina.
ReplyDeleteNimeshitushwa sana na kifo cha Rafiki yangu mpenzi Annastazia! nawapa pole ndugu, jamaa na marafiki MUNGU awatie nguvu kwenye kipindi hiki kigumu.
ReplyDeletebwana ametoa, bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe.
AMEN
Pole sana Brother Isaac. Mungu aipumzishe roho yake mahali pema na awape faraja katika kipindi hiki kigumu.
ReplyDeleteYasini Mfunda