Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel aliyesimama akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa semina ya siku mbili kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Benjamin William Mkapa leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Bibi Mwinda Kiula Mfugale, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Bibi Mizinga Melu na kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Benjamini William Mkapa Mwl. Gebo Steven Lugano.
Meneja Mkuu wa Masuala ya Jamii kutoka benki ya NBC akitoa mada kuhusu namna ya kuweka akiba kwa manufaa ya baadaye kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa leo jijini jijini Darc es Salaam.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Benjamin William Mkapa akichangia mada wakati wa mafunzo kuhusu umuhimu wa kuweka akiba benki, mafunzo ambayo wanafunzi hao wanawezeshwa na wafanyakazi wa benki ya NBC.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel mwenye suti nyeusiakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya umuhimu wa kuweka akiba benki mafunzo ambayo yanaendeshwa na wafanyakazi wa benki ya NBC kote nchini.Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Bibi Mwinda Kiula Mfugale, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Bibi Mizinga Melu.Kutoka kushoto ni Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Benjamini William Mkapa Mwl. Shanina Athman na Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Gebo Steven Lugano.PICHA NA MAELEZO.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...