Mhudumu wa gari la kutolea huduma za afya linalotembea (mobile
clinic) la Benki ya NBC, Wilbard Kiria (kushoto) akimpa mtoto
Shackshazi Rahim dawa ya minyoo katika kliniki ya wamama na watoto
iliyokuwa ikiendeshwa na wahudumu wa gari hilo katika eneo la Kunduchi
Beach nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Gari hilo ni moja ya
magari matano yaliyotolewa kwa Bodi ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam
ili kutoa huduma za afya bure kwa wamama na watoto maeneo ya vijijini.
Mtoto mkazi wa Kunduchi, Rukia Ramadhani akipimwa uzito katika
kliniki ya wamama na watoto iliyokuwa ikiendeshwa na wahudumu wa gari
la kutolea huduma za afya linalotembea (Mobile Clinic) la Benki ya NBC
mahali hapo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Gari hilo ni
moja ya magari matano yaliyotolewa kwa Bodi ya Afya ya Mkoa wa Dar es
Salaam ili kutoa huduma za afya bure kwa wamama na watoto maeneo ya
vijijini. Anayempimawa pili kulia ni muuguzi wa gari hilo, Eliza
Shayo.
Mhudumu wa gari la kutolea huduma za afya linalotembea (mobile
clinic) la Benki ya NBC, Wilbard Kiria (kushoto) akimpa mtoto Gift
Lucas dawa ya minyoo katika kliniki ya wamama na watoto iliyokuwa
ikiendeshwa na wahudumu wa gari hilo katika eneo la Kunduchi Beach nje
kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Gari hilo ni moja ya magari
matano yaliyotolewa kwa Bodi ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam ili
kutoa huduma za afya bure kwa wamama na watoto maeneo ya vijijini.


Hongera NBC!
ReplyDeleteNi muhimu na Mabenki mengine na Mashirika mengine yakawafikia wananchi maeneo ya pembezoni na Vijijini kwa kuwapa huduma za Kihisani za Matibabu.
Pamoja tutaijenga Tanzania!
This is very impressing jamani. Na serikali ingetafuta mabingwa kuzunguka vijijini huko kwa huduma kama hii hata kama ni mara moja kwa mwaka tungeokoa maisha ya kina mama hasa saratani ya maziwa na shingo ya uzazi. magonjwa haya sasa yameenea dunia nzima na tunajua kuwa early detecttion is the key for survival. Mungu awabariki.
ReplyDelete