Mhudumu wa gari la kutolea huduma za afya linalotembea (mobile clinic) la Benki ya NBC, Wilbard Kiria (kushoto) akimpa mtoto Shackshazi Rahim dawa ya minyoo katika kliniki ya wamama na watoto iliyokuwa ikiendeshwa na wahudumu wa gari hilo katika eneo la Kunduchi Beach nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Gari hilo ni moja ya magari matano yaliyotolewa kwa Bodi ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam ili kutoa huduma za afya bure kwa wamama na watoto maeneo ya vijijini.
Mtoto mkazi wa Kunduchi, Rukia Ramadhani akipimwa uzito katika kliniki ya wamama na watoto iliyokuwa ikiendeshwa na wahudumu wa gari la kutolea huduma za afya linalotembea (Mobile Clinic) la Benki ya NBC mahali hapo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Gari hilo ni moja ya magari matano yaliyotolewa kwa Bodi ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam ili kutoa huduma za afya bure kwa wamama na watoto maeneo ya vijijini. Anayempimawa pili kulia ni muuguzi wa gari hilo, Eliza Shayo.
Mhudumu wa gari la kutolea huduma za afya linalotembea (mobile clinic) la Benki ya NBC, Wilbard Kiria (kushoto) akimpa mtoto Gift Lucas dawa ya minyoo katika kliniki ya wamama na watoto iliyokuwa ikiendeshwa na wahudumu wa gari hilo katika eneo la Kunduchi Beach nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Gari hilo ni moja ya magari matano yaliyotolewa kwa Bodi ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam ili kutoa huduma za afya bure kwa wamama na watoto maeneo ya vijijini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera NBC!

    Ni muhimu na Mabenki mengine na Mashirika mengine yakawafikia wananchi maeneo ya pembezoni na Vijijini kwa kuwapa huduma za Kihisani za Matibabu.

    Pamoja tutaijenga Tanzania!

    ReplyDelete
  2. This is very impressing jamani. Na serikali ingetafuta mabingwa kuzunguka vijijini huko kwa huduma kama hii hata kama ni mara moja kwa mwaka tungeokoa maisha ya kina mama hasa saratani ya maziwa na shingo ya uzazi. magonjwa haya sasa yameenea dunia nzima na tunajua kuwa early detecttion is the key for survival. Mungu awabariki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...