Wanariadha wa Polisi Tanzania walioshika nafasi ya kwanza mpaka ya tano katika mbio za Km 12 (Cross Counrty) pamoja na mwalimu wao Naasi Gwagwe wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mbio hizo katika chuo cha Polisi Nchini Namibia wakati wa Michezo ya Nane ya Umoja wa wakuu wa Polisi kwa Nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO).
Wanariadha wa Polisi Tanzania walioshika nafasi ya kwanza mpaka ya tano katika mbio za Km 12 Cross Counrty (walioshika bendera) wakiwa katika picha ya pamoja na washabiki wao baada ya kumaliza mbio hizo katika chuo cha Polisi Nchini Namibia wakati wa Michezo ya Nane ya Umoja wa wakuu wa Polisi kwa Nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO).(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia).
Hatimaye Michezo ya nane ya Umoja wa wakuu wa Polisi kwa Nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO) inatarajiwa kufikia kilele chake kesho huku Wanariadha wa Tanzania wakihitimisha kwa kishindo baada ya kutawala mbio za KM 12 (Cross country) kwa kunyakua nafasi ya kwanza hadi ya tano.

Wanaridha waliofanya vyema na nafasi zao katika mabano ni pamoja Fabian Nelson (1) muda wa dakika 35:36:20 ,Basil John (2), muda wa dakika 35:38:81,Silvester Simon (30) muda wa dakika 36:42:56,Wilbaldo Peter (4) muda wa dakika 36:48:22, na Osward Revelian (5) muda wa dakika 37:36:20

Kwa matokeo hayo mpaka sasa Polisi Tanzania imefikisha jumla medali 15,huku Dhahabu 6,Fedha 4,Shaba 5 ambapo katika ufungaji hapo kesho medali zinatarajiwa kuongezeka kutokana na kuwa na wanariadha wengi waliofanya vizuri pamoja na matokeo katika mchezo wa vishale(dats).

Kwa upande wa Mpira wa miguu, timu ya Polisi Tanzania imeishia katika hatua ya robo fainali baada ya kukubali kichapo cha magoli 2 kwa 1 dhidi ya Afrika Kusini hivyo fainali itachezwa kati ya Afrika Kusini na Zimbabwe huku mpira wa miguu kwa wanawake fainali itachezwa kati ya Kongo na Angola.

Mpira wa pete timu ya Polisi Tanzania imeshika nafasi tano huku Polisi Swaziland ikishika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Zimbabwe, Zambia na Afrika kusini.

Kwa mujibu wa Mwalimu wa Riadha Polisi Tanzania Naasi Gwagwe wanamichezo wa riadha wamefanya vizuri kutokana na kuzingatia mazoezi hasa wakati wa kambi yao waliyokuwa wameiweka katika chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi (MPA) kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mbona hawaonekani katika anga la kimataifa? Michezo ya ubingwa wa dunia imemalizika wiki chache zilizopita ncjini Urusi, hakuna hata mtanzania mmoja aliyewakirisha au umahiri wetu unakomea hapa hapa nyumbani na katika nchi za jirani?

    ReplyDelete
  2. Huu muda waliotumia kukimbia Cross Country umbali wa kilometre 12 inafaa wote wawezeshwe kushiriki mashindano ya kimataifa.

    Maana bingwa wa sasa wa dunia muda wake ni dakika 32: sekunde 45 (32:45)http://www.iaaf.org/competitions/iaaf-world-cross-country-championships.

    Shirikisho la Riadha Tanzania RT/AT mnaona wakimbiaji hawa wa kutuletea medali kimataifa na heshima kwa Tanzania kama Ethiopia, Kenya n.k wanavyofanya kweli.

    Mdau
    Medali Inawezekana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...