Mkazi wa Makumbusho Isabela Edwad Msemo akipokea funguo ya Bajaji akiwa mwenye furaha kutoka kwa Meneja Chapa wa Tigo, Wiliam Mpinga  mara baada ya kujishindia  kupitia Promosheni ya Miliki Biashara yako na Tigo ambapo washindi wa wiki ya pili  wamekabidhiwa zawadi zao jana Jijini Dar es Salaam. 
  Evelyn Elisalia Massawe-(22) Mkazi wa Kimara akipokea funguo za Bajaji mpya aliyojishindia kupitia Promosheni ya Miliki Biashara yako na tTgo kutoka kwa Meneja Chapa wa Tigo Wiliam Mpinga ambapo washindi wa wiki ya pili ya Promotion hiyo wamekabidhiwa zawadi  zao jana Jijini Dar es Salaam.
 Evelyn Elisalia Massawe-(22) Mkazi wa Kimara akishuka ndani ya bajaji yake aliyokabidhiwa na Tigo  baada ya kujishindia kupitia Promosheni ya Miliki Biashara yako na Tigo, kushoto ni  Meneja Chapa wa Tigo Wiliam Mpinga.

 Mkazi wa Mabibo Khalid Jafari Gomani akikagua Bajaji  mpya aliyojishindia kupitia Promosheni ya Miliki Biashara yako na Tigo ambapo washindi wa wiki ya pili ya wamekabidhiwa zawadi zao jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo Wiliam Mpinga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Si kumpa Bajaj tu, hakikisheni anayo leseni halali kabla hajaingia njiani isje kuwa majanga.

    ReplyDelete
  2. Hiyo promotion ni watu wa DSM tu.Huwa kuna jambo moja silieelewi, promotion zilizo nyingi hasa za mitandao ya simu washingi wengi hutokea DSM...ni kwa nini? au mikoani watu hawachangakii hizi fursa...

    ReplyDelete
  3. Duhhh kweli tiGO mmefanya kweli!

    Kwa kweli wasichana wamejikomboa na upandaji wa mabasi na kudhalilika kwa Lifti za watu wenye mashariti magumu.

    Kibongo Bongo umiliki wa Bajaji si haba.

    ReplyDelete
  4. Mdau wa Kwaqnza umenena,

    Lingine zaidi ya Leseni halali ni vipimo vya Kiafya kama Macho, Magonjwa ya Kiasili au ya kuzaliwa na Netiwork zao vichwani!

    Ni ajabu na kweli Dunia nzima Tanzania ndio nchi pekee haina utaratibu wa kuwapima Madereva afya zao mara kwa mara.

    Bongo Jambaland, Bongotambarale ukishapewa Gamba au Leseni ndio imetoka milele na milele, hata kama utapata Utaahira ahalan wasalan utakaa barabarani ukiendesha gari weee hadi siku Kichwa kitakapo panda moto zaidi utakapokuwa hushikiki kwa Uchizi ndio utany'anganywa Funguo za gari!

    ReplyDelete
  5. Mbona mshindi ni mrembo sana!

    ReplyDelete
  6. Ni jambo la muhimu sana mdau amegusia kuhusu kupima madereva afya zao (hasa afya za akili) kaka michuzi kwa nini usite hii kwenye globu ijadiliwe?mimi nadhani unaweza kutumia forum hii kufikisha maoni ya wananchi juu ya baadhi ya kero,ukizangatia kwamba mitandao hii sasa inatambulika. Iweke hii tujadili,ajali zinatokea wakati mwingine kwa kuwa madereva wameshabaki tu na leseni ila wamepoteza sifa zote za udereva,mfano kuona, akili timamu nk.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...