Baadhi ya Wasanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva ambao wanakwenda kutumbuiza kwenye tamasha la Fiesta 2013,linalorajiwa kufanyika Agosti 17,kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma a.k.a Mwisho wa Reli wakiwa kwenye kaburi la Msanii mwenzao,Marehemu Albert Mangwea mapema leo asubuhi kwenye makaburi ya Kihonda,nje kidogo ya mji wa Morogoro, walipokwenda kuzuru na kumuombea dua,walipokuwa wakielekea Mkoani Kigoma.Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amen-
Home
Unlabelled
wasanii watakaotumbuiza tamasha la fiesta 2013 mkoani kigoma wazuru kaburi la marehemu albert Mangwea mapema leo mkoani morogoro.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Jamani watu kwanini hawamuachi huyu kaka wa watu apumzike kila kukicha watu makaburini nendeni kimyakimya basi lazima kupiga picha???
ReplyDeleteSio vibaya kutembelea lakini tunarudi pale pale tabia yetu ya kuonyesha majonzi na mapenzi pale mtu anapokufa sio nzuri.Tunatakiwa kumjali mtu akiwa miza na kumsaidia kwa hali na mali ili awe katika hali nzuri tuwache tabiya ya kumsema akikupa kisogo na kumkwepa.Nani kati ya hawa alishawahi kujaribu kumsaidia katika hili tatizo lake? Je kama uliwahi na kushindwa ulishawahi kuwaomba watu wengine msaidiane kuongea nae.?Tujifunze hapa.
ReplyDelete