Mfanyakazi
wa Inayojiita kampuni ya kukusanya Ushuru ya MTAA WA OYSTERBAY BEACH
PARKING, ambaye hakutaka kutaja jina lake akiandika risiti ya ushuru wa
maegesho ili kuweka katika moja ya gari lililokuwa katika ufukwe wa Coco
Beach, ili alipwe ushuru wa maegesho hayo kiasi cha Sh. 1000 kila gari.
Mfanyakazi huyo alipohojiwa na mtandao huu alisema kuwa anauwezo wa
kukusanya hadi magari 20 kwa siku jambo ambalo si la kweli kwani kwa
muda mchache tu alishapitia magari zaidi ya hayo.
Na
alipoulizwa zinapopelekwa fedha hizo baada ya kukusanywa alisema ''Mimi
sijui zinapopelekwa kwani mimi ni mfanyakazi tu na
nikishakusanya nampelekea Bosi ndo anajua zinapokwenda, kwa siku naweza
kukusanya ushuru hadi wa magari kama 15 hivi,kwa sababu sipo peke yangu
tupo wengi katika eneo hili lote''. alisema mfanyakazi huyo.
Hata
hivyo baadhi ya watu waliokuwapo ufukweni hapo, walisikika wakin'gaka
kutoa ushuru huo, huku wakimhoji ''Tutoe ushuru wa Parking kwa lipi,
hata usafi tu hamfanyi nyie mnajua kuchukua hela tu, na kwanza
mlishazuiliwa kukusanya pesa hizi bado tu mnaendelea na wizi wenu''.
alisikika akilalama jamaa mmoja
Imeelezwa
kuwa Kampuni hiyo inayojishughulisha na kukusanya ushuru huo,
ilishawahi kuwa na mgogoro kipindi cha nyuma, ambapo wahusika waliwahi
kukamatwa na kufikishwa hadi Kituo cha Polisi na kuzuiliwa kufanya kazi
hiyo, kutokana na kutokuwa na ruhusa ya kufanya hivyo na kwamba
hawatambuliki na Halmashauri wala serikali, lakini wanaendelea kinyemela
na kufanya baadhi ya watu wanaowafahamu kuwagomea kutoa ushuru huo
wanapofuatwa kulipia parking hiyo.
Na hata ukiitazama kwa makini Risiti hii haionyeshi
Adress kamili ya wahusika, haina mhuri wala namba za simu zaidi ya
kuandika jina la Serikali ya Mtaa wa Oysterbay Beach, Sasa kuna kila
haja ya kuwahoji Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo ili kujua Mapato na
Matumizi ya ukusanyaji wa Ushuru huu, unaokusanywa kuanzia Jumatatu hadi
Jumapili bila kupumzika na zinapokwenda Fedha hizo.
Hii
ndiyo Risiti yenyewe inayotolewa baada ya kutoa Sh. 1000 kwa
mkusanyaji, ambaye pia anakuwa ameambatana na vijana wawili waliovalia
kiraia Jinzi na Tisheti na makofia ya Sweta, wakimlinda mkusanyaji huyu
mdada na kupiga mkwara kwa anayeonekana kukaidi kutoa Buku.
Mkusanyaji
akiandika Risiti hiyo, ambayo hata akiisha ichana haibaki Kopi yake
kuonyesha kilichoandikwa, Yaani ni Vishina kwa kwenda mbele.
Akienda kuweka risiti katika gari
Akitimiza wajibu wake kuweka katika gari....
Mtoza ushuru hatauona ufalme wa mbinguni?
ReplyDeleteMara kwa mara twasoma habari kama hizi kutoka huko Bongo. Jee hakuna idara maalum inayahusika na kulinda haki za wananchi naona kuna wajanja wengi kazi zao ni kama pick pockets tu.
ReplyDeleteukusanyaji wa ushuru kwa magari yanapoegesha maeneo yeyote iwe ufuko wa bahari au mijini ni Sawa kabisa. Hata nchi zilizoendelea zinafanya hivyo,tena kwa ushuru mkubwa saana kiasi wemgi wanafanya maamuzi kutumia "baiskeli" wakati wa hali ya jua "summer" na vyombo vya usafiri wa umma "Trains,Metro na Mabasi ya umma" wakati wa baridi"winter" kinachotakiwa serikali au kampuni binafsi kuboresha kwa kutumia vyombo vya kisasa(Electronic)vya maandishi na picha ya magari na namba zake
ReplyDeletekwa kupeleka moja kwa moja maelezo ya magari na ukusanyaji wa mapato badala ya njia zinazotumika kwa sasa zinatia wasiwasi wa wajanja kutumia vitabu vya "ukusanyaji bandia" wahusika serikalini au kampuni binafsi tumepitwa na mida ya "manual" mandishi ya mkono tujiunge na maendeleo ya vyombo vya kisasa kuepukana na ghasia.
Mikidadi-Denmark
Huo ni wizi mdogo mdogo unaoendelea hadi UFISADI wa nji yetu. Zitto, tafadhali tusaidie kwa hili pia!
ReplyDeleteWatanzania inbidi tuelimishwe kuwa ni lazima tulipe ushuru na kodi mbalimbali kwa manufaa yetu sisi wenyewe. Tunalalamika sasa tusipopata huduma za jamii kama vile maji safi, umeme, barabara, walimu wa kutosha mashuleni, hospitali nzuri nk. Huduma hizo zina gharama zake. Wakati huo huo tukitozwa kodi tunakuja juu. We can't get both ways. We either have to pay taxes and government dues in exchange for social servises, or refuse to pay and stop complaining against the government. Tusiwe ombaomba wa kutegemea wafadhili ambao misaada yao siyo tu haitoshi, bali inakuja na masharti magumu, mfano ndoa za jinsia moja. Kinachoshauriwa hapa ni kuwapatia UNIFORMS au mavazi maalumu (dress code) na vitendea kazi hawa wakushanyaji wa mapato ili kuwatofautisha na vibaka. Pili polisi wetu wanaovaa kiraia na kubeba SMG mitaani hawana tofauti na majambazi. Ingependeza kama wangevaa bullet proof zenye maandishi (reflectors) POLISI mgongoni na pia wazingatie usafi wa mwili, nywele (grooming), mavazi na wasivae malapa. Wajitambulishe na kuonyesha bedge zao kabla ya kutoa vitisho ili kupata ushirikianao toka kwa raia wema. Mungu wabariki walipa kodi wa Tanzania.
ReplyDeleteTatizo sio kukusanya kodi,mtoa mada anasema hakuna record ya malipo hayo.
ReplyDeleteJe kama hakuna copy ya risiti ya malipo nani anajua huyo dada akakusanya kiasi gani????
Je hiyo serikali ya O/bay inahahakishaje malipo yote yamewafikia ???
Naona hapa hawa wanaokusanya ndio mapato yao,kwani hakuna wa kuhakikisha mapato.
Tunaomba makusanyo yawasilishwe panapo husika na tuone maendeleo kama ulinzi na usafi wa fukwe za bahari.
Serikali yeyote duniani mostly inaendeshwa kwa pesa za walipa kodi raia wema. Hata mataifa tajiri yanopotoa misaada kwa mataifa maskini, ni pesa iliyokusanywa toka kwa walipa kodi wao. Watz tuone aibu, tusipende kulalamikia kila jambo. Tulipe kodi na ushuru ili kuiwezesha serikali yetu kutuhudumia.
ReplyDeleteHILI MBONA ZITTO KABWE ALISHALIZUNGUMZA JUZI TU KWAMBA SERIKALI INAPOTEZA BILIONI 700 KWA UKUSANYAJI WA USHURU WA KUANDIKA KWA MKONO.NI KUTOTAKA KUSIKIA TU KUNAKOFANYWA NA HAO WAVAA SUTI.
ReplyDeleteWatanzania wenzangu, tujaribu kuheshimu watu hata kama hatupendi kazi wanazofanya. Huyu dada ameajiliwa kutoza ushuru. Tunapompiga picha na kusema kuwa anachokifanya ni wizi, ujanja, pickpocketer au ufisadi, tunao ushahidi wa maneno tunayosema? Misaada tunayopata toka nchi za magharibi mingi inatokana na kodi na ushuru kama hou kwa raia zao. Mbona hatuikatai kwa visingizio kuwa kuwa imekusanya na mafisadi, wezi, wajanja ama pickpoketers? Kuipenda nchi yako ni pamoja kulipa kodi na ushuru kwa muda na viwango vinavyotakiwa. Tuelimike na kuheshimu kazi za watu.
ReplyDeletemi yamenikuta tena hata ukisimama tu uwe hauna shida eneo hilo ili mradi umepaki tu gari yako anakuja huyu dada kwa kweli sio siri ninakereka hebu wadau tusaidieni kwa hili
ReplyDeleteKudadadeki!!! Hii ndio Bongo bwana.
ReplyDeleteIsingekuwa vibaya kama ingeenda ktk hiyo serikali ya mtaa wa oysterbay parking...kama upo basi..na ikafanya shughuli za usafi, ulinzi nk. Mdau wa denmark hapo beach sio tu panalindwa bali huduma za afya zipo pia..bure! Tanzania kwa sasa hivi unaweza kufanya kitu chochote tu. Alimradi una mtu. Wa kukulinda. Unakuwa traffic, unakuwa polisi,unafungua hospital na kutoa huduma kubwa bila utaalam, unakuwa usalama wa taifa. Hivi karibuni haya yote yalutokea. Tatizo ni mfumo wa serikali.
ReplyDeleteMFANYA KAZI HANA UNIFORM ...! RECITE IKIJA MVUA INALOWA. SO MUHIME .MPIJAJI TICKET AWE NA UNIFORM KITAMBULISHO ! KISHA RECITE IWE KWENYE KAVA YA LAYLONI NA IWE NA GUNDI AKIIWEKA INATE .
ReplyDeleteYANGU NI HAYO
Kwa nini Hakuna Mashine za TRA za kutoa Risiti hapo?
ReplyDeleteMnakusanya fedha, JE KODI MNALIPA?
Dalili za haraka haraka kwa jinsi zilivyo Risiti hizo hao wooote ni wachumia tumbo!
I smell a rat
ReplyDeleteHapa naona viongozi wa serikali ya mtaa hilo eneo watupe maelezo kamili kuhusu hili suala
ReplyDelete