Mfanyakazi wa Inayojiita kampuni ya kukusanya Ushuru ya MTAA WA OYSTERBAY BEACH PARKING, ambaye hakutaka kutaja jina lake akiandika risiti ya ushuru wa maegesho ili kuweka katika moja ya gari lililokuwa katika ufukwe wa Coco Beach, ili alipwe ushuru wa maegesho hayo kiasi cha Sh. 1000 kila gari. Mfanyakazi huyo alipohojiwa na mtandao huu alisema kuwa anauwezo wa kukusanya hadi magari 20 kwa siku jambo ambalo si la kweli kwani kwa muda mchache tu alishapitia magari zaidi ya hayo.

Na alipoulizwa zinapopelekwa fedha hizo baada ya kukusanywa alisema ''Mimi sijui zinapopelekwa kwani mimi ni mfanyakazi tu na nikishakusanya nampelekea Bosi ndo anajua zinapokwenda, kwa siku naweza kukusanya ushuru hadi wa magari kama 15 hivi,kwa sababu sipo peke yangu tupo wengi katika eneo hili lote''. alisema mfanyakazi huyo.

Hata hivyo baadhi ya watu waliokuwapo ufukweni hapo, walisikika wakin'gaka kutoa ushuru huo, huku wakimhoji ''Tutoe ushuru wa Parking kwa lipi, hata usafi tu hamfanyi nyie mnajua kuchukua hela tu, na kwanza mlishazuiliwa kukusanya pesa hizi bado tu mnaendelea na wizi wenu''. alisikika akilalama jamaa mmoja

Imeelezwa kuwa Kampuni hiyo inayojishughulisha na kukusanya ushuru huo, ilishawahi kuwa na mgogoro kipindi cha nyuma, ambapo wahusika waliwahi kukamatwa na kufikishwa hadi Kituo cha Polisi na kuzuiliwa kufanya kazi hiyo, kutokana na kutokuwa na ruhusa ya kufanya hivyo na kwamba hawatambuliki na Halmashauri wala serikali, lakini wanaendelea kinyemela na kufanya baadhi ya watu wanaowafahamu kuwagomea kutoa ushuru huo wanapofuatwa kulipia parking hiyo.

Na hata ukiitazama kwa makini Risiti hii haionyeshi Adress kamili ya wahusika, haina mhuri wala namba za simu zaidi ya kuandika jina la Serikali ya Mtaa wa Oysterbay Beach, Sasa kuna kila haja ya kuwahoji Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo ili kujua Mapato na Matumizi ya ukusanyaji wa Ushuru huu, unaokusanywa kuanzia Jumatatu hadi Jumapili bila kupumzika na zinapokwenda Fedha hizo. 
 Hii ndiyo Risiti yenyewe inayotolewa baada ya kutoa Sh. 1000 kwa mkusanyaji, ambaye pia anakuwa ameambatana na vijana wawili waliovalia kiraia Jinzi na Tisheti na makofia ya Sweta, wakimlinda mkusanyaji huyu mdada na kupiga mkwara kwa anayeonekana kukaidi kutoa Buku.
 Mkusanyaji akiandika Risiti hiyo, ambayo hata akiisha ichana haibaki Kopi yake kuonyesha kilichoandikwa, Yaani ni Vishina kwa kwenda mbele.
 Akienda kuweka risiti  katika gari
 Akitimiza wajibu wake kuweka katika gari....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Mtoza ushuru hatauona ufalme wa mbinguni?

    ReplyDelete
  2. Mara kwa mara twasoma habari kama hizi kutoka huko Bongo. Jee hakuna idara maalum inayahusika na kulinda haki za wananchi naona kuna wajanja wengi kazi zao ni kama pick pockets tu.

    ReplyDelete
  3. ukusanyaji wa ushuru kwa magari yanapoegesha maeneo yeyote iwe ufuko wa bahari au mijini ni Sawa kabisa. Hata nchi zilizoendelea zinafanya hivyo,tena kwa ushuru mkubwa saana kiasi wemgi wanafanya maamuzi kutumia "baiskeli" wakati wa hali ya jua "summer" na vyombo vya usafiri wa umma "Trains,Metro na Mabasi ya umma" wakati wa baridi"winter" kinachotakiwa serikali au kampuni binafsi kuboresha kwa kutumia vyombo vya kisasa(Electronic)vya maandishi na picha ya magari na namba zake
    kwa kupeleka moja kwa moja maelezo ya magari na ukusanyaji wa mapato badala ya njia zinazotumika kwa sasa zinatia wasiwasi wa wajanja kutumia vitabu vya "ukusanyaji bandia" wahusika serikalini au kampuni binafsi tumepitwa na mida ya "manual" mandishi ya mkono tujiunge na maendeleo ya vyombo vya kisasa kuepukana na ghasia.
    Mikidadi-Denmark

    ReplyDelete
  4. Huo ni wizi mdogo mdogo unaoendelea hadi UFISADI wa nji yetu. Zitto, tafadhali tusaidie kwa hili pia!

    ReplyDelete
  5. Watanzania inbidi tuelimishwe kuwa ni lazima tulipe ushuru na kodi mbalimbali kwa manufaa yetu sisi wenyewe. Tunalalamika sasa tusipopata huduma za jamii kama vile maji safi, umeme, barabara, walimu wa kutosha mashuleni, hospitali nzuri nk. Huduma hizo zina gharama zake. Wakati huo huo tukitozwa kodi tunakuja juu. We can't get both ways. We either have to pay taxes and government dues in exchange for social servises, or refuse to pay and stop complaining against the government. Tusiwe ombaomba wa kutegemea wafadhili ambao misaada yao siyo tu haitoshi, bali inakuja na masharti magumu, mfano ndoa za jinsia moja. Kinachoshauriwa hapa ni kuwapatia UNIFORMS au mavazi maalumu (dress code) na vitendea kazi hawa wakushanyaji wa mapato ili kuwatofautisha na vibaka. Pili polisi wetu wanaovaa kiraia na kubeba SMG mitaani hawana tofauti na majambazi. Ingependeza kama wangevaa bullet proof zenye maandishi (reflectors) POLISI mgongoni na pia wazingatie usafi wa mwili, nywele (grooming), mavazi na wasivae malapa. Wajitambulishe na kuonyesha bedge zao kabla ya kutoa vitisho ili kupata ushirikianao toka kwa raia wema. Mungu wabariki walipa kodi wa Tanzania.

    ReplyDelete
  6. Tatizo sio kukusanya kodi,mtoa mada anasema hakuna record ya malipo hayo.
    Je kama hakuna copy ya risiti ya malipo nani anajua huyo dada akakusanya kiasi gani????
    Je hiyo serikali ya O/bay inahahakishaje malipo yote yamewafikia ???
    Naona hapa hawa wanaokusanya ndio mapato yao,kwani hakuna wa kuhakikisha mapato.
    Tunaomba makusanyo yawasilishwe panapo husika na tuone maendeleo kama ulinzi na usafi wa fukwe za bahari.

    ReplyDelete
  7. Serikali yeyote duniani mostly inaendeshwa kwa pesa za walipa kodi raia wema. Hata mataifa tajiri yanopotoa misaada kwa mataifa maskini, ni pesa iliyokusanywa toka kwa walipa kodi wao. Watz tuone aibu, tusipende kulalamikia kila jambo. Tulipe kodi na ushuru ili kuiwezesha serikali yetu kutuhudumia.

    ReplyDelete
  8. HILI MBONA ZITTO KABWE ALISHALIZUNGUMZA JUZI TU KWAMBA SERIKALI INAPOTEZA BILIONI 700 KWA UKUSANYAJI WA USHURU WA KUANDIKA KWA MKONO.NI KUTOTAKA KUSIKIA TU KUNAKOFANYWA NA HAO WAVAA SUTI.

    ReplyDelete
  9. Watanzania wenzangu, tujaribu kuheshimu watu hata kama hatupendi kazi wanazofanya. Huyu dada ameajiliwa kutoza ushuru. Tunapompiga picha na kusema kuwa anachokifanya ni wizi, ujanja, pickpocketer au ufisadi, tunao ushahidi wa maneno tunayosema? Misaada tunayopata toka nchi za magharibi mingi inatokana na kodi na ushuru kama hou kwa raia zao. Mbona hatuikatai kwa visingizio kuwa kuwa imekusanya na mafisadi, wezi, wajanja ama pickpoketers? Kuipenda nchi yako ni pamoja kulipa kodi na ushuru kwa muda na viwango vinavyotakiwa. Tuelimike na kuheshimu kazi za watu.

    ReplyDelete
  10. mwassy ayoubAugust 22, 2013

    mi yamenikuta tena hata ukisimama tu uwe hauna shida eneo hilo ili mradi umepaki tu gari yako anakuja huyu dada kwa kweli sio siri ninakereka hebu wadau tusaidieni kwa hili

    ReplyDelete
  11. Kudadadeki!!! Hii ndio Bongo bwana.

    ReplyDelete
  12. Isingekuwa vibaya kama ingeenda ktk hiyo serikali ya mtaa wa oysterbay parking...kama upo basi..na ikafanya shughuli za usafi, ulinzi nk. Mdau wa denmark hapo beach sio tu panalindwa bali huduma za afya zipo pia..bure! Tanzania kwa sasa hivi unaweza kufanya kitu chochote tu. Alimradi una mtu. Wa kukulinda. Unakuwa traffic, unakuwa polisi,unafungua hospital na kutoa huduma kubwa bila utaalam, unakuwa usalama wa taifa. Hivi karibuni haya yote yalutokea. Tatizo ni mfumo wa serikali.

    ReplyDelete
  13. MFANYA KAZI HANA UNIFORM ...! RECITE IKIJA MVUA INALOWA. SO MUHIME .MPIJAJI TICKET AWE NA UNIFORM KITAMBULISHO ! KISHA RECITE IWE KWENYE KAVA YA LAYLONI NA IWE NA GUNDI AKIIWEKA INATE .

    YANGU NI HAYO

    ReplyDelete
  14. Kwa nini Hakuna Mashine za TRA za kutoa Risiti hapo?

    Mnakusanya fedha, JE KODI MNALIPA?

    Dalili za haraka haraka kwa jinsi zilivyo Risiti hizo hao wooote ni wachumia tumbo!

    ReplyDelete
  15. I smell a rat

    ReplyDelete
  16. Hapa naona viongozi wa serikali ya mtaa hilo eneo watupe maelezo kamili kuhusu hili suala

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...