Mrembo Clara Bayo akipunga mkono mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Taji la Redd's Miss Tanzania Sports Woman 2013 wakati wa tamasha la michezo la warembo wanao wania taji la Miss Tanzania 2013. Bayo alifanya vyema katika michezo kadhaa na kujizolea point nyingi na kuwashinda warembo wengine 29.
Kwa Taji hilo Clara Bayo ambaye anatoka Kanda ya Ilala, amekuwa mrembo wa nne kuingia nusu fainali za Mashindano hayo makubwa ya urembo nchini ambayo fainali zake zitafanyika Ukumbi wa Mlimani City Septemba 21 mwaka huu.
Clara Bayo akipozi kwa picha.
Warembo walichuana vikali kaika soka huku timu za Redd's na Zanzi zikichuana na Zanzi iliyoongozwa na nahodha na mfungaji bora Happines Watimanywa ikishinda kwa goli 2-1.
Michezo mingine mbalimbali ilifanyika kama kukimbia, kukimbia na magunia, kuruka chini, Volleyball na kuogelea ilifanyika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...