Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kulia) akizindua rasmi kiapo cha utii kwa Wahandisi Wataalamu leo jijini Dar es Salaam kilichofanyika katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wahandisi 2013. Picha kushoto ni Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini Mhandisi Steven Mlote, (katikati) ni Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Wariyaruandwe Lema.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kulia) akimkabidhi cheti pamoja na luptop Anna Msigwa mmoja ya mhandisi mhitimu aliefanya vizuri zaidi katika mtihani wa mwisho wa mwaka 2012/ 2013, (Pichani mwenye kipaza sauti) Ni Msajili wa Bodi ya Wasajili Mhandisis Steven Mlote.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kulia) akimpatia cheti Mhandisi mhitimu Nora Abdalla kati ya aliefanya vizuri zaidi katika mitimani yao ya mwaka wa mwisho2012/2013. (katikati)Masjili wa Bodi ya Wahandisi Mhandisi Steven Mlote.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Wariyaruandwe Lema(kulia) akiwaapisha Wahandisi mbalimbali kutoka taasisi na mashirika ya kihandisi,leo jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya wahandisi 2013 leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahandisi wakila kiapo cha utii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wahandisi waliohudhuria hafla ya maadhimisho ya siku ya Wahandisi 2013 leo jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (hayupo pichani.)Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. jina la mheshimiwa limekosewa hapo katika heading si maguli ni magufuli

    ReplyDelete
  2. WAHANDISI:

    Sio mle Viapo mbele ya Sheria halafu tena mje kujenga nje ya Mashariti na Kanuni za Kisheria na Viwango !!!

    ReplyDelete
  3. safi saana akina dada, mnaweza bila kuwezeshwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...