Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi (CHADEMA), Mhe John Shibuda (katikati) akikumbatiana kwa furaha na Katibu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana alipohudhuria mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Stendi Kuu ya Mabasi ya Mwanhuzia, wilayani Meatu, Mkoa wa Simiyu.Kulia ni Katibu wa tikadi na Uenezi, Ndugu Nape Nnauye.Katika mkutano huo Mhe Shibuda alisema kuwa viongozi wa vyama vya siasa wasilumbane kwa matusi bali washindane kwa hoja.
Mhe John Shibuda akisindikizwa na wafuasi wa chama chake cha CHADEMA kuingia kwenye mkutano wa hadhara wa CCM.
Nape akikumbatiana na Shibuda
Nape akikumbatiana kwa furaha na Nape
Nape akitangaza uwepo wa Shbuda katika mkutano huo
Wafuasi wa CCM wakishangilia wakati Shibuda akihutubia katika mkutano wa CCM
Shibuda na Kinana wakiwatuliza mzuka wafuasi wa vyama hivyo viwili waliopagawa wakati Shibuda akihutubia
Ndugu Kinana akimsindikiza Mhe Shibuda baada ya mkutano huo kumalizika. Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA
itabidi kamati kuu ya chama (Chadema) imuulize alipeleka hoja gani huko, ameleta hoja gani toka ktk mkutano huo. na je? alipata ruhusa ya kamati kuu Chadema kwenda kukutana na viongozi wa CCM.....he may be a traitor.
ReplyDeleteMhe. Shibuda alikuwa sahihi, Hajavunja sheria za nchi. Na kikubwa sisi wakulima wa pamba, pamba ndo kila kitu kuliko hata hizo harakati.
ReplyDeleteKama alivyoeleza alikuja kujadili na kuleta hoja za kuboresha bei ya pamba kwetu sisi wakulima Shibuda yupo sahihi sana tu.nuL