Mtanzania Adubo M. Omar aliefariki dunia tangia Aug 26, 2013,yupo Montuary Dallas Texas nchini Marekani.Mdau Frank Maji ambaye ametuletea habari hizi amesema Marehemu alishawahi ishi miji ya Cedar Rapids na, Des Moines iliyopo Iowa nchini Marekani kabla hajahamia Dallas, Texas ambako mauti ilimkuta taarifa ilizidi kusema marehemu alizaliwa April 25, 1956 kama kuna yeyote anayemfahamu marehemu tafadhali wasiliana na Frank Maji kwa barua pepe fmaji@hotmail.com au simu 214 674 6666 Sikiliza mazungumuzo kuhusu marehemu kati ya Vijimambo na Fank Maji hapo chini
Home
Unlabelled
MTANZANIA ADUBO M. OMAR AFARIKI DUNIA TANGIA AUG 26, 2013 NA NDUGU ZAKE HAWAJULIKANI WALIPO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Poleni sana!! ingekuwa vyema mngeambatanishwa na picha ya marehemu kwa utambuzi zaidi.
ReplyDeleteMaana wasafiri wengine hubadili majina yao ya asili.
Ninavyoelewa ni kwamba hili neno 'tangia' halipo katika lugha ya Kiswahili, kama ni hivyo kwa nini tunapenda kulitumia? Tafadhali Ankal zuia hii code mixing & code switching ya lugha adhimu ya Kiswahili na hivyo vilugha vya makabila mengine, Kiswahili kiwe huru!!!
ReplyDeleteTafadhali weka picha yake itakua rahisi kumtambua, ni rahisi mtu kubadili jina
ReplyDelete