Mtanzania Adubo M. Omar aliefariki dunia tangia Aug 26, 2013,yupo Montuary Dallas Texas nchini Marekani.Mdau Frank Maji ambaye ametuletea habari hizi amesema Marehemu alishawahi ishi miji ya Cedar Rapids na, Des Moines iliyopo Iowa nchini Marekani kabla hajahamia Dallas, Texas ambako mauti ilimkuta taarifa ilizidi kusema marehemu alizaliwa April 25, 1956 kama kuna yeyote anayemfahamu marehemu tafadhali wasiliana na Frank Maji kwa barua pepe fmaji@hotmail.com au simu 214 674 6666 Sikiliza mazungumuzo kuhusu marehemu kati ya Vijimambo na Fank Maji hapo chini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Poleni sana!! ingekuwa vyema mngeambatanishwa na picha ya marehemu kwa utambuzi zaidi.
    Maana wasafiri wengine hubadili majina yao ya asili.

    ReplyDelete
  2. Ninavyoelewa ni kwamba hili neno 'tangia' halipo katika lugha ya Kiswahili, kama ni hivyo kwa nini tunapenda kulitumia? Tafadhali Ankal zuia hii code mixing & code switching ya lugha adhimu ya Kiswahili na hivyo vilugha vya makabila mengine, Kiswahili kiwe huru!!!

    ReplyDelete
  3. Tafadhali weka picha yake itakua rahisi kumtambua, ni rahisi mtu kubadili jina

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...