Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo , Prof. Elisnate Ole Gabriel, (kulia) akiongea na Bondia Mstaafu Rashid Matumla(wenye fulana ya mistari) leo jijini Dar es Salaam, ambapo ametakiwa kurithisha kipaji chake kwa vijana nchini (kushoto) ni Mkurugenzi wa Michezo katika wizara hiyo Leonard Thadeo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ,Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akiongea na Bondia Mstaafu ,Rashid Matumla leo jijini Dar es Salaam alipomtembelea,(Pichani mwenye koti jeusi) Mkurugenzi wa Michezo katika wizara hiyo, Leonard Thadeo,(mwenye fulana ya mistari) ni Bondia Mstaafu Rashid Matumla,.. (kushoto) Afisa Vijana katika wizara hiyo Amina Sanga.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) pamoja na Bondia Mstaafu Rashid Matumla (mwenye fulana ya mistari ) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Michezo katika Wizara hiyo Leonard Thadeo(kushoto) wakati akitoa maelezo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye miwani) Mkurugenzi wa Michezo katika wizara hiyo Leonard Thadeo( mwenye koti jeusi kulia), Bondia Mstaafu Rashid Matumla (mwenye fulana ya mistari)), pamoja na Afisa Vijana katika wizara , Amina Sanga(kushoto). Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO

Na Concilia Niyibitanga

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imemtaka Bw. Rashid Matumla ambaye ni bondia mstaafu katika mchezo wa ngumi za ridhaa kurithisha kipaji chake kwa vijana wengine.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Prof Elisante Ole Gabriel wakati akiongea na Bw. Matumla alipomtembelea ofisi kwake.

Prof. Gabriel amemtaka kuanzisha kikundi cha vijana ambacho ataweza kukifundisha mchezo huo ili kipaji chake kisipotee ukizingatia kuwa Tanzania ina wachezaji wachache katika mchezo huo.

“Ni vema ukarithisha ujuzi wako katika mchezo wa ngumi kwa vijana chipukizi kwa kuwafundisha na kuwashauri katika mchezo huo” Amesema Prof. Gabriel.

Amesema kuwa Serikali inatambua mchango wake katika mchezo wa ngumi hapa nchini na hivyo si vema akakaa na ujuzi wake ukizingatia kuwa yeye amestaafu katika mchezo huo.

Aidha, Prof. Gabriel ameongeza kuwa kwa kufanya hivo Matumla atawasaidia vijana chipukizi kuwa Mabondia wazuri wa baade ikiwa ni pamoja na kujiajiri badala ya kujihusisha na vitendo vibaya kama matumizi ya madawa ya kulevya n.k

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Bw. Leonard Thadeo amesema kuwa kikundi hicho kinaweza pia kikajihusisha na ujasiriamali kwa kuomba mikopo katika Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa kuwa wanamichezo pia wanatakiwa kujishughulisha na ujasiriamali ili kujiongezea kipato.

Kwa upande wake Bw. Matumla amesema kuwa amefurahi na amefarijika sana kuongea na viongozi wa wizara inayosimamia michezo na vijana kwa kuwa wameonesha kutambua mchango alioliletea Taifa hili katika mchezo huo.

Matumla amesema kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha kuwa anawarithisha mabondia chipukizi na vijana wengine kipaji chake katika mchezo huo ili wawe mabondia bora wa baadaye.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hapa sielewi, Rashid alikuwa bondia mzuri sana matunda yake yako wapi? Yaani kwa bongo ni kwamba michezo hailipi. Ona hao wengine kwenye picha wanavyopendeza wakati Rashid amechooka. Kama serekali inania ya kuendeleza mchezo wa ngumi basi ifanye hivyo, itengeneze ukumbi wa ngumi, waweke vifaa vinavyotakiwa, then wamuajiri kwa mshahara mzuri Rashid awe kocha. Hapo ndio ataweza kurithisha kipaji chake, tena inabidi mumuombe maanake sio lazima.

    ReplyDelete
  2. Binafsi nilidhani kua,Matumla anakabidhiwa boxing gym ili aweze kurithisha kipaji chake kumbe alikua akipewa usia kwamba asikae bure aendeleze vipaji vya watoto kwa njia na uwezo anaoujua yeye!!!!!ama kweli hii bongo, basi hapo wameshategesha wanasubiri msaada toka nje wa kujengewa gym.Binafsi naungana na mchangiaji wa kwanza hapo juu kwamba, jengeni gym kuubwa kisha muajirini Matumla awe mwalimu hii pia ni njia mojawapo ya kuthamini mchango wake kwa Taifa.

    ReplyDelete
  3. Je Mzima huyo au kama Mohamen Ally?

    ReplyDelete
  4. Serikali inamuwezesha vipi ili awezeshe wengine??? Ni majuzi tu tulisikia matumla analia njaa, sasa atawezeshaje wengine wakati nyumbani kwake njia ya chooni imeota majani????!!! Tuache siasa bali tutende

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...