Serikali imeyafungia  kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba,2013  kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala  za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.

Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba,2013.Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali(Government Notice )Namba 333 la tarehe 27 septemba,2013.

Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani,mfano tarehe 17 Julai,2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013”  kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri  haukupaswa kuchapishwa Magazetini.

Aidha, katika toleo la Jumamosi,tarehe 17 Agosti,2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI”  habari hiyo ilikolezwa na picha ya mbwa  mkali mwenye hasira.Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka Mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya kiislam.Jambo ambalo halikuwa la  ukweli.

Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti.Serikali na jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi lake haliwezi kupitisha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.

Hivyo basi,kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya kiislam  mbwa ni najisi hapaswi kuingia  katika maeneo ya ibada.

Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini(90) kuanzia tarehe 27 Septemba,2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi.Gazeti hili limeonywa mara nyingi  lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa  kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za  fani ya Habari.

Pamoja na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti, mfano ;katika toleo na 7262 la 20 Machi,2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA DAMU”,tarehe 12 Juni,2013,toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.

Aidha, siku ya Jumatano,tarehe 18 Septemba,2013 katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha Kichwa cha habari kisemacho “SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta  kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika .Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika  na wahanga waliomizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na  waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.

Vile vile gazeti hilo limeishtumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.

Kwa ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama  wavione kuwa haviwasaidii.

Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu serikali imelifungia gazeti la Mtanzania  kutochapishwa kwa muda wa siku tisini(90) kwa Tangazo la Serikali Namba 332(Government Notice No.332) la tarehe 27 septemba,2013,.
Serikali inawataka wamiliki,wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa makini,kuzingatia weledi,miiko na madili yataaluma uandishi wa habari.

Serikali inawataka wamiliki na hasa wahariri kuhakisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia taaluma,kuweka mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu.

Serikali inavionya vyombo vya habari vinavyoutumia uhuru wa habari bila wajibu kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwemo ya kuvifungia .Serikali haitakubali kuona vyombo vya habari kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani  nchini.
Imetolewa na


MKURUGENZI IDARA YA HABARI
WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
28 SEPTEMBA,2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. duh! kuandika habari zinazoigusa serikali imekuwa ni shubiri.

    ReplyDelete
  2. Haya magazeti mm nahisi wamiliki wao au waandishi wao sio WATANZANIA tunaomba watu wa operesheni KIMBUNGA waingie huko kuwasaka ndugu zangu watanzania tuilindeni nchi yetu kwa udi na uvumba na amani yetu pia,wamiliki wa vyombo vya habari muwe makini mnapoajili wafanyakazi muwe wazalendo kwa wazawa na mchunguzane wenyewe kwa wenye msitoe chance kwa mamluki muwe makini na hao WAHAMIAJI HARAMU,mm naipenda nchi yangu ya TANZANIA,je vipi? Nyie wandishi wa habari,naitwa mdudu kakakuona,napatikana huku UINGEREZA,nakupendeni woote huko nyumbani,

    ReplyDelete
  3. Nashangaa hamkuwapiga faini, tena nzito, na kuwapa muda mfupi wa kuilipa.

    ReplyDelete
  4. mwananchi lipi

    mbona nalipata hapa ubungo

    http://www.mwananchi.co.tz/

    ReplyDelete
  5. wmananchi ni gaziti la wakenya!!!

    ReplyDelete
  6. Freedom of speech is under attack in tanzania,

    ReplyDelete
  7. Freedom of opinion and speech by any means should be accompanied by discipline and maximum accountability. What has been done is absoultely correct though it has taken so long for the government to act on this press misbehaviour due to its tolerance!!!

    ReplyDelete
  8. Wajinga ndio waliwao nyie mwananchi mnawaamsha vipi waliolala,andikeni Habari wanazozipenda kuhepusha dhahama hizi, wacha watanzania waishi gizani

    ReplyDelete
  9. Wangeyafunga kabisa na kurudi masikani kenya,adhabu waliopewa ni ndogo kufuatana na mtazamo wa magazeti haya kwa kuwapotosha viongozi na jamii. Hata nchi zilizoendelea kuna uhuru wa wanahari kutopangiwa mipaka lakini wanajiwekea mipaka ya kueshimu serikali na jamii badala ya kubomoa na kupotosha. Amani kwanza
    Mickey"mikidadi"Jones
    denmark

    ReplyDelete
  10. mambo ya nchi za dunia ya tatu hayo..hawaangalii hata maslahi ya waajiriwa wa hilo gazeti na familia zao...kwani kulikuwa hakuna jinsi nyingine ya kuliadhibu hilo gazeti zaidi ya kulifungia ? Bongo tuache mizengwe...Mbona serekali haijasema ukweli ambao wao inaoudhania ? nje ya topiki hii..michuzi weka contacts zako tukupe habari kutoka huku Canada...kuna habari muhimu sana kuhusu ndugu zetu na mambo ya biashara haramu..juzi wamekwisha..picha zao kila kona ya habari hapa..tv/radio/ magazeti...Noma..

    ReplyDelete
  11. Mdau hapo juu endelea kuishi denmark tuache sisi Tuitetee Tanzania yetu kwa nguvu zote. Wewe si uko nje ya nchi ndo mana unashabikia vitendo vibaya vya vyombo vya habari kikinuka hapa wewe haupo? Sisi tunazungumzia Taifa wewe unazungumzia familia ya mtu mmoja????

    ReplyDelete
  12. Serikali iendelee kuvifungia vyombo vyote ambavyo havina maadili, tunaona yanayoendelea huko duniani tuweni makini mataifa meengi yanatamani sana amani yetu ivunjike. Hao mburura wanaoandika hizo habari sio watanzania

    ReplyDelete
  13. Hivi mishahara ya watumishi wa serikali inayotokana na sisi walipa kodi mbalimbali kwa Serikali Kuu na Serikali za mitaa ili watupatie huduma wananchi wa Tanzania nayo ni sirikali?

    Mimi mlipa kodi ningetaka kujua watumishi wa umma tunawalipa kiasi gani ikiwemo mishahara, marupurupu na bonsai.

    Mdau
    Mlipa-Kodi

    ReplyDelete
  14. Yes!! They're supposed to report responsibly, this should be a lesson to other tabloids.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...