Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe kuelekea ukumbini kutunukiwa Shahada Ijumaa Septemba 20, 2013.
Nyimbo za taifa zikipigwa wakati wa sherehe za kumtunuku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aki Shahada ya Uzamivu katika Chuo Kikuu Guelph jimboni Ontario, Canada, Ijumaa Septemba 20, 2013.
Sehemu ya umati ulioshuhudia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitunukiwa Shahada ya Uzamivu na Provost na Makamu wa Rais wa Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario, Dkt Maureen Mancuso , Ijumaa Septemba 20, 2013.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Hongera sana DR.JAKAYA KIKWETE.
ReplyDeleteTUNAFARIJIKA SANA NA MAFANIKIO YAKO NDANI NA NJE YA MIPAKA YETU.
HONGERA KWA TUZO HII.
Mdau UK
Hongera JK !
ReplyDeleteUnatutoa Kimasomaso kila uendapo, je ndugu zako Maraisi wenzako wa hii Afrika ya Mashariki Kundi la akina K-3 namna gani?, wao hawasomi ama kuonekana na heshima zozote?, au ndio wao ni vilaza?
Kikwete DUME bana:
ReplyDeleteKenya, Rwanda na Uganda mmeliona 'Jembe' la Afrika ya Mashariki?
Sio jingine ila ni Raisi Jakaya Kikwete wa Tanzania!!!
Hongra sana Mh. Dr Jakaya Kikwete kwa tunzo hii ya Phd. Tunafarijika sana kuona mafinikio yako mema ya ndani na nje ya nchi yetu. Shughuli imependeza Masha Allah. Hongera sana.
ReplyDeleteMaryam Seif
Essex UK
Msisahau alipata PhD nyingine toka Chuo kikuu cha Uturuki,akapata Marekani na hata Nairobi University walimpatia baada ya kuwasuluhisha magomvi yao ya Kikabila.ambapo waliuana kama Kuku.
ReplyDeleteHongera JK.
Safia H.K
Bromley-UK