Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe kuelekea ukumbini kutunukiwa Shahada Ijumaa Septemba 20, 2013.
Nyimbo za taifa zikipigwa wakati wa sherehe za kumtunuku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aki Shahada ya Uzamivu katika Chuo Kikuu Guelph jimboni Ontario, Canada, Ijumaa Septemba 20, 2013.
Sehemu ya umati ulioshuhudia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitunukiwa Shahada ya Uzamivu na Provost na Makamu wa Rais wa Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario, Dkt Maureen Mancuso , Ijumaa Septemba 20, 2013.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hongera sana DR.JAKAYA KIKWETE.
    TUNAFARIJIKA SANA NA MAFANIKIO YAKO NDANI NA NJE YA MIPAKA YETU.
    HONGERA KWA TUZO HII.
    Mdau UK

    ReplyDelete
  2. Hongera JK !

    Unatutoa Kimasomaso kila uendapo, je ndugu zako Maraisi wenzako wa hii Afrika ya Mashariki Kundi la akina K-3 namna gani?, wao hawasomi ama kuonekana na heshima zozote?, au ndio wao ni vilaza?

    ReplyDelete
  3. Kikwete DUME bana:

    Kenya, Rwanda na Uganda mmeliona 'Jembe' la Afrika ya Mashariki?

    Sio jingine ila ni Raisi Jakaya Kikwete wa Tanzania!!!

    ReplyDelete
  4. Hongra sana Mh. Dr Jakaya Kikwete kwa tunzo hii ya Phd. Tunafarijika sana kuona mafinikio yako mema ya ndani na nje ya nchi yetu. Shughuli imependeza Masha Allah. Hongera sana.

    Maryam Seif
    Essex UK

    ReplyDelete
  5. Msisahau alipata PhD nyingine toka Chuo kikuu cha Uturuki,akapata Marekani na hata Nairobi University walimpatia baada ya kuwasuluhisha magomvi yao ya Kikabila.ambapo waliuana kama Kuku.
    Hongera JK.
    Safia H.K
    Bromley-UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...