ZAIDI ya washiriki 100 kutoka ndani na nje ya nchi watashiriki
kwenye tamasha la Sanaa na utamaduni la Jambo Festival litakalofanyika oktoba
23 hadi 27 mwaka huu katika viwanja vya Suye vilivyopo Arusha.
Mwenyekiti wa tamasha hilo, Augustine Namfua alisema kuwa tamasha hilo ni la pili
kufanyika mkoani Arusha ambapo wamekuwa wakifanya kila mwaka lengo likiwa ni
kuwawezesha washiriki mbalimbali kuweza kuonyesha bidhaa zao za
kitamaduni kutoka ndani na nje ya nchi.
Alisema kuwa tamasha hilo la kimataifa pia litawashirikisha
washiriki kutoka nchi za Ufaransa na Angentina ambao wataonesha mambo mbalimbali na kuonyesha bidhaa zao za
kitamaduni .
Alisema tamasha hilo litaenda sambamba na matukio mbalimbali ya kiasili
ikiwemo maonyesho ya mavazi ya kiasili, pamoja na tamasha la kiasili
kutoka vikundi vya miji ya Tanga, Arusha, na Dar es Saalamu .
Namfua aliongeza pia
kutakuwepo na tamasha la muziki wa kisasa pamoja na onesho
la mavazi, na ubunifu wa mavazi ambapo kwa
siku hizo kila siku kutakuwa na matamasha mbalimbali.
Amesema maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika kwa asilimia 50 huku watu
mbalimbali wakiwemo watu binafsi, mashirika na taasisi mbalimbali zinazohusika na
maswala ya sanaa na tamaduni wanaendelea kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya
kushiriki.
"Tamasha la mwaka jana lilifana sana
kwani tuliweza kupata washiriki wengi sana kutoka ndani na nje ya nchi na
lilikuwa na mwitiko mkubwa sana , huku watu mbalimbali wakipata fursa ya
kuonyesha sanaa zao na tamaduni mbalimbali na kuweza kujifunza kutoka kwa
wenzetu wa nje ya nchi ndio maana tumeamua kufanya tena mwaka huu mwezi wa kumi
hivyo tunatarajia watu mbalimbali kushiriki kikamilifu katika tamasha
hilo’alisema Namfua.
Aidha aliwataka watu mbalimbali kufika
katika tamasha hilo na kuonyesha bidhaa zao za kitamaduni
zinazotengenezwa kwa mikono pamoja na kutangaza tamaduni zao za Kiafrika na kuwataka wadau mbalimbali kuonyesha moyo katika kusaidia matamasha
hayo ili yaendelee kufanyika mara kwa mara.
good job Augustine
ReplyDeleteHongera sana Augustine.....All the best
ReplyDelete