Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles
Tizeba akizungumza na Kaimu Mkuu wa Bandari ya Mwanza, Bw. Edwin Kasyupa
(kushoto) wakati alipotembelea Banda la TPA katika kilele cha maadhimisho ya
siku ya Bahari Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Bandari ya Mwanza North.
Wakazi wa Mwanza wakipata maelezo
mbalimbali kuhusu mipango ya kuendeleza Bandari katika maziwa makuu wakati
walipotembelea banda la TPA katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Bahari
Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Bandari ya Mwanza North
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa TPA, Joseph
Msaki akisikiliza jambo kutoka kwa mmoja wa wawakilishi wa taasisi
zilizoshiriki maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani yaliyofanyika katika viwanja
vya Bandari ya Mwanza North.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles
Tizeba akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya usafirishaji majini
wakati wa kongamano la kuadhimisha siku ya Bahari Duniani lililofanyika jijini
Mwanza.
Habari na Picha na
Afisa Mawasiliano wa TPA Focus Mauki
Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeshiriki maadhimisho ya siku ya Bahari
Duniani yaliyofanyika jijini Mwanza katika viwanja vya Bandari ya Mwanza North.
Umoja wa
Mataifa kupitia Shirika lake la Bahari Duniani (IMO) linaadhimisha Siku ya
Bahari Duniani, Septemba 26 kila mwaka.
Maadhimisho
hayo hufanyika mara moja kila mwaka ambapo pamoja na mambo mengine Jumuiya ya
Kimataifa ya Bahari ikiongozwa na Shirika la Bahari Duniani (IMO), huyaadhimisha
kwa kutathimini usimamiaji wa ulinzi, usalama na utunzaji wa mazingira baharini
na katika maziwa.
Tanzania
ikiwamo nchi nyingine wanachama wa IMO huadhimisha siku hii kwa kufanya maonyesho
ya siku mbili ambayo huandaliwa na SUMATRA. Kwa mwaka huu maonyesho haya yamefanyika
Septemba 25 na kufikia kilele chake Septemba 26 mwaka huu.
Pamoja na
kuwa na maonyesho kwa umma, SUMATRA iliandaa kongamano lililofanyika Septemba
26 ambalo lililenga kuonyesha mchango wa Sekta ya Bahari na Bandari katika
kukuza na kuleta maendeleo endelevu hapa nchini.
Kaulimbiu
katika maadhimisho ya mwaka huu ni, ‘Maendeleo endelevu: Mchango wa IMO
kupitia Agenda ya Rio +20’. Kwa mujibu wa SUMATRA kauli mbiu ya mwaka huu imechaguliwa
kuonyesha mchango wa IMO kwa mwaka 2013 katika kubeba jukumu la kutekeleza
makubaliano ya kimataifa juu ya kuleta maendeleo endelevu yaliyoafikiwa katika
kikao kilichofanyika Juni 20 hadi 22, 2012, Rio de Janeiro, Brazil
kijulikanacho kama ‘Rio+20’.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Alhaj Ahmad Kilima amenukuliwa na vyombo vya habari
akisema Umoja wa Mataifa umechukua hatua za kimaendeleo kwa kuweka malengo
mengi ili kufikia maendeleo endelevu ambayo hayatoathiri uwezo wa dunia, mfumo
asilia pamoja na kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi zinazoikabili jamii.
Sekta ya
bahari ina mchango mkubwa katika mihimili mitatu ya maendeleo endelevu ambayo
ni uchumi, jamii na utunzaji wa mazingira ya bahari. Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari Tanzania (TPA) inaendelea na mikakati mbalimbali ya kuboresha Bandari
zake kote nchini, ili imeweka mazingira na miundombinu ya kisasa itakayotoa mchango
katika kufikia malengo yaliyopo kitaifa na kimataifa.
|
siku ya bahari au bandari, kwani mwanza kuna bahari, wanasheherekea bahari au ziwa?
ReplyDelete