Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Pascal Lesoinne
(kulia) akimkabidhi Redds Miss Tanzania Happiness Watimanywa mfano wa hundi wakati akimkabidhi msaada wa mifuko 300 ya saruji kwa ajili ya
ujenzi wa shule ya watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino)
itakayojengwa mkoani Shinyanga. wa pili kushoto ni Mkuu wa itifaki wa
Miss Tanzania, Albert Makoye na Meneja Mahusiano ya Jamii wa Twiga
Cement, Natasha D’souza. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jijini Dar
es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Pascal Lesoinne
(kulia) akimkabidhi Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige mfano wa hundi
wakati akimkabidhi msaada wa mifuko 600 ya saruji kwa ajili ya ujenzi
wa shule na zahanati zitakazojengwa mkoani Shinyanga. Katikati ni
Meneja Mahusiano ya Jamii wa Twiga Cement, Natasha D’souza. Hafla
ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mshindi wa tatu wa Redds Miss Tanzania 2013, Clara Bayo
akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Twiga Cement, Pascal Lesoinne
wakati wa hafla hiyo. Katikati ni mshindi wa pili, Latifa Mohamed na
kulia ni Redds Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa. Msaada wote
wa mifuko 900 ya saruji unagharimu shs milioni 30.


It's true that 900 bags of Cement cost 30 millions?
ReplyDeleteHapa naona mwandishi kachemka kidogo. Mifuko 900 ya cement inagharimu milioni 30? Kivipi? ina maana kwa wastani mfuko wa cement kutoka kiwandani ni 33,333/- duuuh! mtaani utakuwa bei gani?
ReplyDeleteNdo tatizo la watu alionunuliwa, mifuko 900 eti milioni 30??? juzi tu nimenunua mifuko 250 kwa 4 milioni! 16,00/- each tena Mwanza!
ReplyDeleteMaandishi si kama kuongea tu. Ukikosea ktk maandishi si rahisi kujisahihisha, maana ujumbe ulio ktk maandishi, hata ukisahihishwa makosa, siyo rahisi kwa kila aliyeona ujumbe wa awali kuona pia ujumbe uliosahihishwa.
ReplyDeleteKwa mfano wewe Ichamoyo, umejifanya mjanja sana, kumbe mshamba tu. Unadai umenunua mifuko 250 kwa milioni 4, kila mfuko 16,00/-. Je, unadhani uko sahihi?
Kama hauko sahihi jua na mwenzio kakosea si kwa makusudi, ni kama ulivyokosea wewe.