Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Pascal Lesoinne (kulia) akimkabidhi Redds Miss Tanzania Happiness Watimanywa mfano wa hundi wakati akimkabidhi msaada wa mifuko 300 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule ya watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino) itakayojengwa mkoani Shinyanga. wa pili kushoto ni Mkuu wa itifaki wa Miss Tanzania, Albert Makoye na Meneja Mahusiano ya Jamii wa Twiga Cement, Natasha D’souza. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Pascal Lesoinne (kulia) akimkabidhi Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige mfano wa hundi wakati akimkabidhi msaada wa mifuko 600 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule na zahanati zitakazojengwa mkoani Shinyanga. Katikati ni Meneja Mahusiano ya Jamii wa Twiga Cement, Natasha D’souza. Hafla ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mshindi wa tatu wa Redds Miss Tanzania 2013, Clara Bayo akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Twiga Cement, Pascal Lesoinne wakati wa hafla hiyo. Katikati ni mshindi wa pili, Latifa Mohamed na kulia ni Redds Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa. Msaada wote wa mifuko 900 ya saruji unagharimu shs milioni 30.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. It's true that 900 bags of Cement cost 30 millions?

    ReplyDelete
  2. Hapa naona mwandishi kachemka kidogo. Mifuko 900 ya cement inagharimu milioni 30? Kivipi? ina maana kwa wastani mfuko wa cement kutoka kiwandani ni 33,333/- duuuh! mtaani utakuwa bei gani?

    ReplyDelete
  3. Ndo tatizo la watu alionunuliwa, mifuko 900 eti milioni 30??? juzi tu nimenunua mifuko 250 kwa 4 milioni! 16,00/- each tena Mwanza!

    ReplyDelete
  4. Maandishi si kama kuongea tu. Ukikosea ktk maandishi si rahisi kujisahihisha, maana ujumbe ulio ktk maandishi, hata ukisahihishwa makosa, siyo rahisi kwa kila aliyeona ujumbe wa awali kuona pia ujumbe uliosahihishwa.

    Kwa mfano wewe Ichamoyo, umejifanya mjanja sana, kumbe mshamba tu. Unadai umenunua mifuko 250 kwa milioni 4, kila mfuko 16,00/-. Je, unadhani uko sahihi?

    Kama hauko sahihi jua na mwenzio kakosea si kwa makusudi, ni kama ulivyokosea wewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...