Watanzania wenzetu,
Tunapenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu kwamba Jumamosi hii (i.e. September 28th, 2013) kutakuwa na ufunguzi wa tawi la CCM Ohio kuanzia saa tisa mchana mpaka saa kumi na moja jioni kwenye ukumbi wa Palace The Square ( 5817 Emporium Square, Columbus Ohio 43229)
Mgeni rasmi katika ufunguzi huu atakuwa Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania (pichani).
Hii ni nafasi ya sisi wote kama Watanzania, sio lazima uwe mwanachama wa CCM au chama chcochote cha siasa, kupata fursa ya kukutana na watanzania wenzako kutoka miji mbalimbali ya Ohio na Kiongozi/Viongozi wa nchi yetu.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na
Fredd Mujuni - Mwenyeketi : 216- 225-1585
E. Joe Ngwilizi Muhaya - Katibu Mkuu - 330-361-1933
Kelvin Mkwawa - Katibu mwenezi- 614 -596-3762
Tumaini Mosha - Mjumbe Mkuu - 216- 645-6171
Ahsanteni,
Mungu Ibariki Tanzania
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...