Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA),Juma Pinto akizungumza na Waandishi wa Habari jioni hii nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Water Front,kunakofanyika Uchaguzi wa Rais na viongozi mbali mbali wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) ambapo hadi sasa hakuna Mwandishi yeyote alieruhusiwa kuingia kwenye Ukumbi huo kwa madai kwamba Waandishi hawausiki na Uchaguzi huo,kwani waandishi jukumu lao ni kusubiria kupewa matokeo tu ya uchaguzi huo,kauli iliyotolea na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi,Ndg. Hamidu Mbwezeleni.Jambo hilo liezua tafrani kidogo kwenye Eneo hilo hasa pale Watu wa Usalama (Polisi) walipowataka Waandishi kuondoka kwenye Eneo hilo la Uchaguzi.Mwenyekiti wa TASWA,Juma Pinto amewataka Waandishi wa Habari kuachana na Uchaguzi huo na kutoripoti chochote,kwani kilichoonyeshwa ni dharau kubwa kwa waandishi wa Habari na watanzania wote nchini wanaopenda Michezo.
Home
Unlabelled
Breaking Nyuzzz.....Waandishi wa Habari watimuliwa Uchaguzi wa TFF
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hapo lazima kuna "kitu" kwenye huo uchaguzi.
ReplyDeleteDavid V
inawezekana waandishi walijenga mazoea tu ya kwamba wanastahili kuwepo ndani ya ukumbi, waandishi jengeni utamaduni wa kuheshimu maamuzi halali hasa sheria inapozingatiwa.
ReplyDeleteSidhani kama ni busara sana kufikiri kuwa kitendo cha kuwaondoa waandishi ndani ya ukumbi wa mkutano/uchaguzi inaweza ikatafsiriwa moja kwa moja kuwa ni mizengwe....mizengwe kwanani maana wagombea wote wapo, wapiga kura wapo, kamati ya usimamizi wa uchaguzi wapo....sasa nani amfanyie mizengwe mwingine?
ReplyDeleteWaandishi wetu tunawapenda sana na tunajua mnayo shauku kubwa ya kutuletea "breaking news" toka huko kwenye mkutano wa uchaguzi; lakini wekeni subira ili hatimaye mje mtoe "official report" ya hicho kinyang'anyiro cha uchaguzi.
Yeah....busara ituongoze ndugu waandishi wetu ... tuweke subra!
Wandishi waangalie sheria
ReplyDeleteSheria ya Uchaguzi wa Viongozi wa TFF inasemaje? Sheria ya FIFA ya uchaguzi wa Viongozi wa Vyama vya Michezo kwenye nchi zinasemaje? Kwa nini TFF haikuwapatia elimu au taarifa Waandishi wa Habari mapema kuwa hawatakiwi kuhudhuria uchaguzi huo na kwamba wao wangesubiri kupewa matokeo tu? Je, kwenye shughuli zijazo za TFF, waandishi wa habari wataendelea kupewa tu taarifa na sio kuhudhuria mikutano yao? Yapo maswali mengi yakujiuliza!
ReplyDeleteNiko disguised kidogo na hii misamiati yetu ya 'kwanini hatukupatiwa elimu' au 'kwanini hawakupatiwa elimu'...swali bado liko palepale, je hao waandishi wapokwenda kwenda kwenye huo mkutano wa uchaguzi walifanya matayarisho gani ya kutambua kanuni zinazoendesha uchaguzi? Je wanaweza kutuambia ni kanuni gani ya uchaguzi wa TFF imevunjwa kwa kuwatoa nje ya ukumbi wakati mkutano wa uchaguzi ukiendelea?
ReplyDeleteTusubiri kauli za Mwenyekiti wa Uchaguzi atoe ufafanunuzi juu ya uzingatiwaji wa jambo hili.
Waandishi wetu wa habari hawajui mipaka yao wala kanuni kwani tumeshuhudi waandishi wakidai hata kuingia ndani ya nyumba ya mtu binafsi eti wana haki ya kuandika habari. Uchaguzi unapofanyika hairuhusiwi asiyehusika kuwemo ndani ya chumba cha kupigia kura bali ni wapigakura tu ndio wanaotakiwa. waandishi hawa walichotaka ni baada ya uchaguzi waandike kuwa fulani alimpigia kura fulani ilimradi kuleta mgongano.
ReplyDeleteWaandishi wa bonge wengi wao ni wakurupukaji na wapotoshaji wakubwa, kila mtu anataka aonekane ni wa kwanza kutoa (breaking news) bila hata ya kufanya utafiti wa kina matokeo yake mnaupotosha umma. Hongera TFF kwa kuwatimua hao warudi shule wakajifunge vema maadili ya uandishi.
ReplyDeleteAnonymous No.ameeleza vizuri waandishi wanapaswa kuripoti official report. sasa walitaka kuingia kufanya nini? wao ni wajumbe?. Kama sio kwenda kulikisha vimeseji vya umbea kwenye simu zao. Heshimu taratibu na sheria .
ReplyDelete