Na Abdulaziz Video
Wakuu wa Idara na Vitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi wametakiwa kuacha vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na baadhi ya wakuu hao kwa watumishi wengine wa Kada za Chini na kusababisha kuzorota kwa utendaji wa kazi hali inayosababisha jamii kutopata huduma ipasavyo na kuichukia Seikali yao
Wakuu wa Idara na Vitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi wametakiwa kuacha vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na baadhi ya wakuu hao kwa watumishi wengine wa Kada za Chini na kusababisha kuzorota kwa utendaji wa kazi hali inayosababisha jamii kutopata huduma ipasavyo na kuichukia Seikali yao
Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Mhe Agnes Hokororo katika
kikao cha mwisho kilichofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa
halmashauri baada ya kukamilisha kukutana na watumishi mbalimbali wa
Umma wa halmashauri hiyo
Baadhi ya watumishi hasa wa idara ya elimu walilalamikia vitendo
vinavyofanywa na wakuu wa vitengo na wa idara kuwanyanyasa kwa lugha
chafu hata mbele ya wanafunzi hali hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa
kuzorotesha maendeleo Hususan katika Kada ya ualimu.
Mhe Hokororo alisema kuwa jukumu la viongozi ni kuwa karibu na wale
waliochini yao na kuonesha ushirikiano na ili kuleta ufanisi katika
eneo la kazi na si kuonesha vitendo vya unyanyasaji.
Alimtaka Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,Reuben Mfune
kufuatilia tuhuma hizo na kuwachukulia hatua wale wota watakaobainika
kuwa na tabia za kuwanyanyasa walio chini yao
‘Ded hakika tulikuwa wote kwenye mikutano hii na umesikia mwenyewe
watumishi walivyokuwa wanasema Fanyia kazi na ndio lengo la kufikia na
kupata matokeo bora sasa Imenisikitisha sana kusikia unyanyasi wa
wakubwa wa Idara …Alimalizia Hokororo Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Rueben Mfune aliahidi
kufanyia kazi malalamiko hayo ya watumishi hao na kuwataka watumishi
hao kuendelea na majukumu yao kwa lengo la kufikia ufanisi.
Aidha Mfune alieleza kuwa Halmashauri yake imejipanga kutatua kero za
watumishi ikiwemo vitendea kazi,malazi na Malipo ya usumbufu na Likizo
na kuhimiza watumishi hao kutekeleza wajibu wao ili kuimarisha Wilaya
hiyo inayokuwa kiuchumi
Katika ziara hizo Mkuu wa wilaya aliweza kukutana na watumishi walio
katika kata zote 21 za Wilaya hiyo hivi karibuni
Mkurugenzi mtendaji wa Ruangwa,Rueben Mfune akieleza mipango ya halmashauri hiyo kwa kila kata kwa mwaka huu wa Fedha
Watumishi wa halmashauri ya wilaya kutoka kata 9 za Taraf ya Ruangwa walipokuta na mkuu wa wilaya
Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya wilaya kutoka kata 9 za Taraf ya Ruangwa walipokuta na mkuu wa wilaya


Hata hapo kwenye mkutano vumbi tupu
ReplyDelete