Na Abdulaziz Video
Wakuu wa Idara na Vitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi wametakiwa kuacha vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na baadhi ya wakuu hao kwa watumishi wengine wa Kada za Chini na kusababisha kuzorota kwa utendaji wa kazi hali inayosababisha jamii kutopata huduma ipasavyo na kuichukia Seikali yao
 Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Mhe Agnes Hokororo katika kikao cha mwisho kilichofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa halmashauri baada ya kukamilisha kukutana na watumishi mbalimbali wa Umma wa halmashauri hiyo Baadhi ya watumishi hasa wa idara ya elimu walilalamikia vitendo vinavyofanywa na wakuu wa vitengo na wa idara kuwanyanyasa kwa lugha chafu hata mbele ya wanafunzi hali hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha maendeleo Hususan katika Kada ya ualimu. 
Mhe  Hokororo alisema kuwa jukumu la viongozi ni kuwa karibu na wale waliochini yao na kuonesha ushirikiano na ili kuleta ufanisi katika eneo la kazi na si kuonesha vitendo vya unyanyasaji. Alimtaka Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,Reuben Mfune kufuatilia tuhuma hizo na kuwachukulia hatua wale wota watakaobainika kuwa na tabia za kuwanyanyasa walio chini yao ‘Ded hakika tulikuwa wote kwenye mikutano hii na umesikia mwenyewe watumishi walivyokuwa wanasema Fanyia kazi na ndio lengo la kufikia na kupata matokeo bora sasa Imenisikitisha sana kusikia unyanyasi wa wakubwa wa Idara …Alimalizia Hokororo Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Rueben Mfune aliahidi kufanyia kazi malalamiko hayo ya watumishi hao na kuwataka watumishi hao kuendelea na majukumu yao kwa lengo la kufikia ufanisi. Aidha Mfune alieleza kuwa Halmashauri yake imejipanga kutatua kero za watumishi ikiwemo vitendea kazi,malazi na Malipo ya usumbufu na Likizo na kuhimiza watumishi hao kutekeleza wajibu wao ili kuimarisha Wilaya hiyo inayokuwa kiuchumi Katika ziara hizo Mkuu wa wilaya aliweza kukutana na watumishi walio katika kata zote 21 za Wilaya hiyo hivi karibuni  
Mkurugenzi mtendaji wa Ruangwa,Rueben Mfune akieleza mipango ya halmashauri hiyo kwa kila kata kwa mwaka huu wa Fedha
 Watumishi wa halmashauri ya wilaya kutoka kata 9 za Taraf ya Ruangwa walipokuta na mkuu wa wilaya
Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Mhe Agnes Hokororo akizungumza na Watumishi wa Kata 9 Katika Tarafa ya Ruangwa ikiwa ni mkutano wake wa mwisho kukutana watumishi wa Umma katika wilaya hiyo,Wengine kutoka kushoto ni kaimu Afisa elimu na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bw Rueben Mfune
Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya wilaya kutoka kata 9 za Taraf ya Ruangwa walipokuta na mkuu wa wilaya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hata hapo kwenye mkutano vumbi tupu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...