Siku, miezi na
miaka imepita, leo imetimia miaka Ishirini
na Tano (25) tangu Mwenyezi Mungu akuite nyumbani.
Jumatatu ile
ya majonzi makuu, Bwana alitazama shambani mwake, akaona sehemu iliyo wazi. Kisha
akatazama duniani, na kukuona ukiwa hoi taabani, pale hospitalini. Ndipo
alipokukumbatia na kukuambia “Emmanuel, imetosha, njoo nyumbani”.
Hakika bustani
ya Bwana yapendeza, maana imesheheni watu wake walio bora, wampendezaye.
Ahadi ya Bwana
imetimia, kama yanenavyo maandiko matakatifu kuwa, “…Yeye alisikiaye neno langu
na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele, wala haingii hukumuni,
bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani”. Yohana Mtakatifu 5:24
Nasi tunazidi
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya maisha haya, tangu tulivyokuwa nawe
kimwili hadi sasa ambapo unaendelea kudumu nasi kiroho. Na imani yetu sote
imezidi kuimarika.
Tena
tunamshukuru Mungu kwa baraka na rehema zake zisizo kifani. Tunamshukuru kwa
kutimiza ahadi zake kwetu.
Unakumbukwa
sana na familia yako, ndugu, majirani na marafiki. Mama Salome, watoto wako
wote na wenzi wao, wajukuu zako, dada, kaka na wengine wote wanakukumbuka, kila
mmoja kwa namna ya kipekee.
Kwetu
unaendelea kudumu katika kila pumzi ya uhai wetu. Tunaendelea kusimama katika
misingi uliyoiweka, tena bila kutetereka. Tunakuenzi kwa vitendo, tena bila
kuchoka. Ndio maana tuna kila sababu ya kusherehekea siku hii ya matumaini - tukitumaini
kuwa, siku moja tutaungana nawe katika shamba la Bwana, maskani yetu ya milele.
Hadi
tutakapofika huko, tunazidi kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuilaza roho yako
mahala pema peponi, kwa watakatifu wake. Amen.
Judge Salome kaganda mungu akubariki
ReplyDelete