Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na viongozi
wa Chama Cha Walimu Zanzibar (ZATU), Ofisini kwake Migombani.
Rais wa Chama Cha Walimu Zanzibar (ZATU), Salim Kitwana Sururu (kushoto), akiwasilisha maoni ya chama hicho kwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Ofisini kwake Migombani.
Rais wa Chama Cha Walimu Zanzibar (ZATU), Salim Kitwana Sururu (kushoto), akiwasilisha maoni ya chama hicho kwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Ofisini kwake Migombani.
Baadhi
ya viongozi wa Chama Cha Walimu Zanzibar (ZATU), walimsikiliza Maalim Seif,
walipokutana nae Ofisini kwake Migombani. (Picha na Salmin Said, OMKR).
===== ======= =========
Chama Cha Walimu
Zanzibar (ZATU), kimepongezwa kutokana na uvumilivu walionao katika kutafuta
njia muafaka za kutatua kero zinazowakabili.
Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ametoa pongezi hizo Ofisini kwake
Migombani, wakati akizungumza na viongozi wa
Chama hicho wakiongozwa na Rais wa ZATU, Salim Kitwana Sururu.
Amesema takriban nchi
zote za Afrika Mashariki zimekuwa zikikumbwa na migogoro kati ya serikali na
vyama vya walimu, lakini ni jambo la kufurahisha kuona Chama Cha Walimu
Zanzibar hakiingi katika migogoro hiyo na badala yake kimekuwa kikitumia njia
za Kidiplomasia katika kutatua kero zake.
Amekitaka Chama hicho
kuendeleza moyo huo, kwani njia bora ya kutatua mizozo ni mazungumzo, na wala
sio malumbano au migomo.
Amefahamisha kuwa
uzoefu unaonesha kuwa mara nyingi inapotokea migomo ya walimu linaloathirika ni
Taifa na vijana, na kwamba hakuna haja ya kushiriki au kushabikia malumbano ya
aina hiyo.
Ameeleza kuwa Serikali
kwa upande wake iko tayari kukutana na wadau mbali mbali kujadiliana juu ya
kero zinazowakabili, ili kutafuta njia ya kuzitatua kwa njia ya amani bila ya
kuwepo malumbano.“Hakuna lisilozungumzika,
na mimi nasema njia muafaka ya kutatua kero za namna hiyo ni mazungumzo. Kwa
hivyo endeleeni na moyo huo huo na bila ya shaka kero zenu zitatatuka”, alisema
Maalim Seif kuwambia wakuu wa ZATU.
Kwa upande wake Rais
wa Chama Cha Walimu Zanzibar (ZATU), Salim Kitwana Sururu, amesema ni heshima
kubwa kwa Zanzibar kutokumbwa na migomo ya walimu ambayo imekuwa ikijitokeza
katika nchi jirani mara kwa mara.Ameahidi kuwa ZATU
kitaendelea kutumia njia za mazungumzo katika kutatua kero zinazowakabili, na
kwamba kitafanya hivyo ili kulinda heshima ya Zanzibar.
Naye Katibu Mkuu wa
Chama hicho Mussa Omar Tafurwa, ameiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
kuitekeleza kikamilifu Sera ya Elimu Zanzibar, ili kuleta maendeleo
yaliyokusudiwa katika sekta ya elimu.
Amefahamisha kuwa
bado yapo mambo mengi ambayo hayajatekelezwa ndani ya sera ya elimu ikiwa ni
pamoja na kuanzishwa kwa Mamlaka ya uajiri wa walimu, pamoja na Baraza la
Walimu Zanzibar, mambo ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...