Abas Kinzasa kwa jina la usanii anaitwa 20 Percent akiwa kwenye majonzi baada ya kufiwa na Baba yake mzazi Mzee Kinzasa aliyefariki juzi siku ya Jumapili na kuzikwa siku ya Jumatatu kwenye kijiji cha Kimanzichana kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.
Msanii 20 Percent na ndugu zake wakiweka udongo kwenye kaburi la marehemu baba yake mzazi mzee Kinzasa.
Hii ndio nyumba aliyoicha marehemu Mzee Kinzasa iliyoko kwenye kijiji cha Kimanzichana.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Nyumba ya udongo halafu ya ghorofa!

    ReplyDelete
  2. Pole sn mwanamuziki wa ukweli,lakini nauliza hivi ni nini maana ya zawadi za KIRIMANJORO MUSIC AWARDS? Huyu sialipata tuzo Tano kama sijakosea wadau wote wa bongo flava,sasa hivi hizi tuzo zinakua hazina pesa au malipo? Coz ukipiga mahesabu ya watu walio huzulia kwenye zile tuzo ni wengi sn,,sasa kwani wanamuziki wetu wanakua katika hali ya umasikini kiasi hiki? Wako wapi akina radio mawingu,na wale wanaoandaa zile tunzo,wako wapi wanamuziki kama vile Diamond na wengineo ili wampe sapoti mwenzao,sasa kama mwendo wenyewe ndio huo kwenye muziki wa kitanzania basi bora upigwe malufuku na serikali coz HAUNA FAIDA KWA WANAMUSIC WETU wanaofaidika ni watu wengine kabisaa,hii haikubariki kabisa wanamuziki wote muamke kwenye usingizi mzito,muangalieni mwezenu kwa jicho la tatu kisha mtapata jibu la ukweli,huu ni ushauli wangu kwenu wana BONGO FLAVA,naitwa mdudu kakakuona,nipo huku UINGEREZA,

    ReplyDelete
  3. Je, hii ni ghorofa???

    Pia jamani nyie mapromota na mameneja wa wasanii, jaribuni kuwainua wasanii. Msiwanyonye, mpaka mkakausha damu yote.

    Sasa tazama nyumba ya baba mzazi wa msanii aliyebeba tuzo lukuki za Kili Music. Ni balaa tu.

    Kama wasanii watakuwa ni wapenda starehe, jaribuni kuwa wanonko. Badala ya kuwalipa pesa taslimu muwe mnawawekea vitega uchumi. Kama vile kuwajengea majumba ya kuishi na kupangishä.

    Maana kwa bongo tena, mtu akiwa maarufu kidogo; breakfast, lunch na dinner vyote anapata baa. Huku akitoa ofa lukuki kwa totozi.

    ReplyDelete
  4. R.I.P BABA MZEE KINZASA.
    Poleni saana ndugu wote katika familia ya mzee Kinzasa.Mwenyezi Mungu ndo mpangaji.Tupo Pamoja katika msiba wa mzee wetu Kinzasa.
    mikidadi-denmark

    ReplyDelete
  5. POLE SANA DOGO, MIMI HUAMINI KABISA WAKATI HUU WA MSIBA HUO MZITO , NADHANI UMESHAJUA NANI WA KWAKO. HAO ULIONAO HAPO NDIO NDUGUZO. ACHANA NA WAUZA SURA N.K.MUNGU AWAPE NGUVU.

    ReplyDelete
  6. Mh! Kiswahili cha mchangiaji wa pili hapo ni majanga.
    Hivi kwanini hamjui kutofautisha L na R?!!!

    ReplyDelete
  7. hiyo nyumba ni ya baba yake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...