Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(Mb) mapema leo Oktoba 21, 2013 alipowasili katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro tayari kwa ufunguzi rasmi wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. Wa pili kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kuhusu Maendeleo ya Shirika la Magereza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima( hayupo pichani) kufungua rasmi Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 kinachofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
Baadhi ya wajumbe wanaoshiriki Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa mwaka wa fedha 2013/2014 wakiwemo Wakuu wa Magereza Mikoa yenye miradi ya Shirika pamoja na Wasimamizi Wakuu wa Miradi hiyo wakisikiliza hotuba ya Mgeni katika ufunguzi wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza ambacho kimeanza leo Oktoba 21, 2013 katika Ukumbi wa Edema, Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima( wa tatu kulia) akifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa Bajeti ya Shirika la Magereza kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 leo Oktoba 21, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro( kushoto kwake) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima((wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Magereza yenye miradi ya Shirika mara baada ya kufungua rasmi Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 leo Oktoba 21, 2013 katika Ukumbi wa Edema, Morogoro( wa tatu kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja( wa pili kushoto) ni Kamishna Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile. Wengine ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa( wa pili kulia) na Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga( wa kwanza kulia). Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...