Kampuni ya Strabag imeanza ujenzi wa barabara ya njia nne katika eneo la Kivukoni Front ambalo lina ofisi mbalimbali za Serikali.   Ujenzi huo ulianza jana tarehe 30 Oktoba, 2013. Kwa mujibu wa wajenzi, ujenzi huo utaunganisha Barabara za Kilwa na Morogoro. Aidha inaelezwa kuwa maegesho ya magari yatakuwepo pembezoni mwa barabara  upande wa bahari  ujenzi ukiisha,lakini kwa sasa watu wanapaki maeneo mengine ya mjini.Picha zote na "Bella"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Waendwa-kwa- miguu pia tuwekewe vibaraza vya simenti (pavement)katk njia hii inayotanuliwa.
    Mdau
    Kivukoni Front

    ReplyDelete
  2. wekeni na njia ya baiskeli

    ReplyDelete
  3. Pia wasitusahau wenda kwa miguu na hata waendesha baskeli, mkatuwekea alau vivukio ( Pedestrian Crossings like Pelican, Puffin, Toucan e.t.c.) Mbali ya hizo 'ZEBRA crossings' ambazo hata kuzijali, kuziheshimu na kuzithamini huwa hakupo kwa madereva na si aghlabu hata kuonekana kwa kufukiwa na vumbi/michanga. Naamini taatibu taratibu almuradi hatusimami tutafikia malengo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...