Askari polisi wakiwa na silaha wakiwa wamezingira nyumba iliyokuwa
ikitumika kwa shughuli za kutolea Mimba.
  Daktari mstaafu wa hosptali ya rufaa ya Mawenzi Frances Shayo akiwa
mikononi mwa polisi muda mfupi baada ya kumkamata akitaka kuwatoa
mimba wasichana wawili.
Umati wa watu waliofika katika nyumba ambayo inadaiwa kufanyika
vitendo vya kutoa mimba. Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii  Moshi.
==========   ========   ========
JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kumnasa daktari mstaafu wa hospitali ya rufaa ya Mawenzi,mkoani Kilimanjaro, Frances Shayo(56) akiwa katika harakati za kuwatoa mimba wanawake wawili akiwemo Irene Musa(18) mwanafunzi wa shule ya sekondari Nkwereko iliyoko Masama wilayani Hai.

Daktari huyo ambaye anatajwa kufanya vitendo hivyo mara kwa mara amekamatwa  pamoja na watu wengine watano wakiwa katika nyumba ya mkazi wa Kata ya Ng’ambo aliyefahamika kwa jina moja na  Minde.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema daktari huyo amekuwa akifanya shughuli hiyo kwa muda mrefu katika eneo hilo na mara nyingine amekuwa akifanya shughuli za kuwatairi watoto katika nyumba ya rafiki yake huyo.
Akizungumza na waandishi wa habari daktari Shayo amesema msichana huyo alifika katika nyumba hiyo  akiwa na tatizo la kufunga kutokwa na damu hivyo alikuwa kwenye harakati za kutaka kumsaidia.
Kwa upande wake mama mzazi wa binti huyo,Rozi Urasa amesema alifika nyumbani kwa daktari huyo baada ya kushauliwa na baadhi ya ndugu zake kumpeleka kutoa ujauzito huo kutokana na kwamba huenda binti huyo akakosa kazi pindi atakapokuwa akitafuta kazi akiwa na ujauzito.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ndio maana polisi wetu wana kuwa accused kwa excessive use of force; sasa hapo AK 47 wametinga nazo za kazi gani...unahitaji silaha nzito kiasi hicho kumkamata doctor?????

    ReplyDelete
  2. Polisi watanzania bwana, kweshnei kabisa. Baada ya kwenda na mabunduki kumtafuta jambazi, mnaenda kutamfuta mtu ambaye hana silaha. Kwani anawalazimisha wanawake watoe mimba au wanaenda wenyewe.

    Mdau Kibaha

    ReplyDelete
  3. hili suala la POLISI kuvaa nguo za kawaida naona kama lipitiwe tena linachangia kiasi kikubwa cha ujambazi na kuuawa kwa raia wasio na hatia TANZANIA hatujafikia hayo kwanza

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...