Baadhi ya washiriki wa kozi ya Ukocha Ngazi ya Pili (Intermediate) wakimsikiliza mkufunzi wa kozi hiyo, Rogasian Kaijage (hayupo pichani) Juni mwaka huu.Kozi hiyo iliendeshwa na DRFA.

CHAMA cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kimezitaka timu zinazoshiriki Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha makocha wao wanakuwa na taaluma ya ngazi ya pili (Intermediate) na mikataba ya kazi hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano wa DRFA Kenny Mwaisabula amesema Dar es Salaam kuwa timu zote zinatakiwa kutekeleza agizo ili kuendana na malengo ya chama hicho katika kukuza na kuendeleza mchezo huo.

“Tunazitaka timu zote zinazoshiriki Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam kuwa na makocha wenye taaluma hiyo Ngazi ya Pili (Intermediate), tunafanya hivi ili kuendana na dhamira yetu ya kukuza na kuendeleza mpira wa miguu.

“Kama mtakumbuka vizuri DRFA iliendesha mafunzo ya ukocha wa Ngazi ya Pili (Intermediate) Juni mwaka huu ikiwa na nia njema ya kuhakikisha mafanikio yanapatikana, tumekuwa mstari wa mbele na mfano wa kuigwa katika kuendeleza mpira wa miguu hasa taaluma ya makocha,” alisema.

Alisema timu hizo zimepewa mechi tatu kutekeleza agizo hilo na iwapo hawatatekeleza zitachukuliwa hatua. Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam ilianza Novemba 23 ikishirikisha timu 32.

Kamati ya Mashindano ya DRFA inaongozwa na Mwaisabula, wakati Makamu Mwenyekiti ni Shaaban Mohamed huku wajumbe wakiwa ni Hugo Seseme, Daudi Kanuti, Kassim Mustapha, Abeid Mziba na Bakari Mtumwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...