Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (wa tatu kutoka kushoto)
akikata uteepe kuashiria uzinduzi rasmi wa zoezi la kugawa matrekta ya
mkopo kwa wakulima kutoka wilaya za mkoa wa dodoma, hafla hiyo
ilifanyika leo kwenye ofisi za Kampuni ya NAM Ltd mjini Dodoma ambayo
inakopesha matrekta hayo kwa wakulima, jumla ya matrekta matano yenye
thamani ya shilingi 175,000,000/- yalikopeshwa kwa wakulimaleo hii.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kulia) akimkabidhi funguo ya
trekta mkulima Kalanga Ngudong' wakai wa hafla ya kukabidhi kwa wakulima
matrekta hayo ya mkopo yaliyotolewa na kampuni ya kusambaza matrekta ya
NAM Ltd ya Mjini Dodoma, anayeshuhudia katikati ni mkurugenzi mtendaji
wa NAM Ltd Bw. Aspenas Mwaranga, hafla hiyo ilifanyika leo mjini Dodoma.
Mkulima Kalanga Ngudong' kutoka kijiji cha Magungu Chamwino Dodoma
akiwasha trekta lake alilokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (hayupo
pichani) baada ya mkulima huyo kupata mkopo wa trekta hilo kutoka kwa
kampuni ya NAM Ltd ya mjini Dodoma iinayokopesha matrekta hayo (NAM
Truck), hafla hiyo ya kukabidhi matrekta hayo ilifanyika leo hii kwenye
viwanja vya kampuni ya NAM mjini Dodoma. PICHA NA JERRY MWAKYOMA WA OFISI YA MKUU WA MKOA DODOMA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...