Kamati ya Bingr ya Katiba, Sheria na Utawala iko nchini Kenya kwa ajili ya ziara maalum ya kimafunzo katika Bunge la Jamhuri ya Kenya. Ziara hiyo ya kimafunzo imejikita katika maeneo yafuatayo
(i) Namna Bunge la Kenya linavyofanya kazi katika mchakato wakatiba mpya na utungaji wa katiba
(ii) Ushiriki wa Wananchi katika utungaji wa katiba
(iii) Utaratibu uliyotumika katika kupitisha katiba; na
(iv) Utaratibu wa kura ya maoni ( Referundum)
Ujumbe huo mzito ambao una jumla ua wajumbe 20 unaongozwa na Mh. Pindi Hazara Chana ( Mb), ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba. Wakiwa katika ziara hiyo, wajumbe walipata fursa ya kutembelea ubalozi leo asubuhi na kuonana na Mh. Balozi Batilda S. Brian.
Mh. Batilda S. Birian akitoa taarifa fupi kwa wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu majukumu ya Ubalozi, utendaji na changamoto tunazokumbana nazo katika kufanikisha majukumu ya kila siku.
Mh Balozi Batilda S. Burian akiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Wabunge mara baada ya kupata taarifa ya utendaji wa ubalozi.


.jpg)
.jpg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...